HEMEDY NJE,NI DHIDI YA MTIBWA KESHO

Akizungumza na mbeyacityfc.com muda mfupi uliopita kocha Phiri amesema kuwa maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika kinachosubiriwa ni dakika 90 hapo kesho huko Manungu Complex dhidi ya wenyeji  Mtibwa Sugar.

“Tuko Morogoro, tulifika hapa ijumaa usiku,siku ya jana tulifanya mazoezi kwa saa mbili na baadae vijana wakapata nafasi ya kupumzisha miili kwenye barafu,lengo likiwa ni kuwekana sawa hasa baada ya safari ndefu,leo tumefanya mazoezi ya mwisho kuhakikisha  tuko fiti tayari kwa mchezo wa kesho,morali ni kubwa kambini, tutamkosa Hemedy aliyepata majeraha mchezo uliopita lakini tayari tuna watu ambao watajaza nafasi yake”,  alisema.
City inakutana na Mtibwa Sugar katika mchezo huu wa kufunga duru ya kwanza ya VPL  ikiwa imefanikiwa kukusanya pointi 19 na kushika nafasi ya 8  tofauti ya poingti 1 na timu hiyo ya Manungu iliyo kwenye nafasi ya 6 ikiwa imekusanya pointi 20.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.