MNYAMA SIMBA ACHOMWA MISHIKAKI TAIFA AKIBALI GILI MOJA LA AFRICAN LYON

Timu ya African Lyon imeharibu sherehe za Simba katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam baada ya kuwatandika goli 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara na kuvunja mwiko wa wekundu wa Msimbazi kucheza bila kufungwa.

Kwa matokeo hayo yameifanya Lyon kufunga pazia la mzunguko wa kwanza kwa ushindi mnono na Simba walikuwa wamecheza mechi 13 bila kupoteza hata mchezo mmoja msimu huu.

Aliyepeleka kilio Msimbazi ni kinda la zamani la Yanga B,Abdallah Msuhi dakika za majeruhi  90 baada ya uzembe wa beki pamoja na kipa wa Simba kujichanganya na kumkuta mfungaji katika nafasi nzuri na kuipandisha Lyon nafasi ya tisa wakiwa na pointi zao 17.

Licha ya kufungwa Simba inabaki kileleni mwa msimamo wa Ligi wakiwa na pointi 35 na mchezo wao wa mwisho wa kufunga mzunguko wa kwanza wanaenda kumaliza mkoani Mbeya dhidi timu ya Tanzania Prisons mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine siku ya Jumatano.

Simba wanatarajia kusafiri kesho kuelekea mjini Mbeya kucheza na Prisons ambao nao wamejeruhiwa kwa kufungwa na mabingwa watetezi Yanga goli moja kwa bila lililofungwa na Simon Msuva na kufanya tofauti ya pointi 5 ya Ligi hiyo

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.