Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo ameahidi Neema kubwa kwa walimu na
wanafunzi watakaofanya vizuri katika masomo ya sayansi katika mkoa wa Dar es
salaam akianza na matokeo ya mtihani wa kidato cha nne unaofanyika mwaka huu.
Makonda
amesema kuwa Mwanafunzi wa kidato cha nne katika mkoa wa Dar es salaam
atakayeongoza katika masomo ya sayansi atapata nafasi ya kusoma Bure kidato cha
Tano na cha Sita kwa kulipiwa kila kitu na ofisi ya mkuu huyo wa mkoa na baada
ya kumaliza kidato cha sita Atakayeongoza atapewa Shiling Million Mbili kwa
ajili ya kuanzia maisha yake ya chuo kikuu jambo ambalo Makonda amesema kuwa
analifanya ili kuinua hari ya wanafuzi wa Dar es salaam kupenda masomo ya
sayansi.
Aidha
katika upande wa walimu Makonda amesema kuwa mwalimu wa masomo ya sayansi
ambaye atasaidia shule yake kupata mwanafunzi aliyeongoza katika masomo ya
sayansi mwalimu huyo atapata Shilingi millioni mbili kama zawadi kutoka katika
ofisi yake na pia mwalimu huyo atapewa nafasi ya kuchagua mbuga nzuri yoyote
nchini atakayokwenda yeye na mwenza wake kwa ajili ya kupumzika na kupunga upepo kwa
Siku mbili.
Baadhi ya madwati yaliyotolewa na shule hiyo kama msaada kwa shule za mkoa wa Dar es salaam |
Mh Makonda amesema kuwa kutokana na uhaba mkubwa wa walimu wa sayansi na wataalamu
wengine na ukizingatia kuwa Tanzania inajiandaa kuwa nchi ya viwanda sasa
ameanza Juhudi binafsi kwa ajili ya kuongeza wataalamu wa masomo wa sayansi ili
wawe hazina ya Taifa Baadae.
Ahadi
hizo Amezitoa leo Jijini Dar es salaam wakati akipokea Msaada wa madawati zaidi
ya Mia mbili yenye Thamani ya Million 20 yaliyotolewa na uongozi wa Shule ya
kimataifa ya AL MUNTAZIR SCHOOL ikiwa ni msaada wa kuunga mkono Juhudi za
serikali karika kutatua tatizo la uhaba wa Madawati Katika Jiji hilo.
Mkuu
huyo wa mkoa ameipongeza Shule hiyo kwa Msaada huo ambao utasaidia kupunguza
uhaba wa madawati huku akiwataka wadau wengine kuendelea kuunga mkono Juhudi
hizo kwa maendeleo ya Elimu ya mkoa wa Dar es salaam
na Tanzania
kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment