Thursday, November 3, 2016

TIGO YAJA NA VIFIRUSHI VIPYA VYA INTANETI 'MEGA MIX'

 Ofisa mkuu wa Biashara wa Tigo Shavkat Berdiev (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Kampuni ya Simu ya Tigo kuja na vifurushi vipya vya intaneti ;Mega Mix'. Kulia ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
 Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.



 Na Dotto Mwaibale

Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imetangaza kuanzishwa kwa  ofa ya MEGA MIX ambayo itakuwa inatoa vifurushi vya intaneti ambayo vitawazawadia wateja dakika za ziada kwa ajili ya kupiga simu. Ofa  hii itawapatia wateja  urahisi wa kutumia vifurushi hivi vipya kupitia kifaa chochote kinachotumia intaneti  zikiwemo simu za mkononi  na modemu. 

Akitangaza vifurushi vya Mega Mix kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo Ofisa mkuu wa Biashara wa Tigo Shavkat Berdiev alivielezea vifurushi hivyo  kama “hatua moja mbele ya mabadiliko katika soko  inayotoa   vifurushi sahihi zaidi: ikiwa ni suluhisho kwa watumiaji wote wa data ndani ya sekta ya mawasiliano ya simu nchini Tanzania.”

 Shavkat  aliongeza, “Wateja wetu hivi sasa  wana uhuru wa kuchagua  kutoka katika simu zao  kifurushi chochote wanachokitaka kikiwa na dakika za ziada  zitakazo wawezesha kuunganishwa na wapendwa wao  wakati tunapoukaribisha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.”

 Aliendelea kusema, “Kwa vifurushi vipya wateja wanaweza kuhabarishwa kwa wakati katika mtiririko wa  kuunganishwa  na  wenzi wao na kuwa bega kwa bega na yanayotokea  sehemu mbalimbali duniani. Vifurushi hivi vipya vinaendelea kuonesha jinsi Tigo ilivyojikita katika kuboresha mabadiliko katika mtindo wa maisha ya kidijitali na inavyoongoza katika kutoa  teknolojia ya kisasa pamoja na ubunifu  kwa wateja wetu.

“Wateja wetu vilevile wanaweza kuzipata taarifa za kidunia, kutafuta  kupitia Google, kusikiliza muziki, kuangalia video, kupakua na hata  kutiririsha sinema. Hii ni kwa sababu  tumeunda vifurushi hivi  kwa kuzingatia mahitaji ya kipekee ya wateja  wetu  kwa kufanya uwepo urahisi katika kuchagua  kutoka  katika kifurushi kimoja  kwenda kingine kutegemeana na hali ya kifedha ya wateja.”

Aidha Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga alisema, “Kutokana na teknolojia ya 4G LTE kupatikana  kwa hivi sasa katika miji 20 vifurushi vya  Mega Mix  kunafungua enzi mpya za kufikia intaneti kusiko na ushindani, ambako kutaondoa vikwazo  na kuwawezesha watumiaji  kuona mengi, kusikia zaidi na hatimaye  kupata yaliyo mazuri katika maisha.”

Mpinga aliongeza, “Mteja anachotakiwa kukifanya ili kupata  vifurushi vya Mega Mix ni kupiga  *148*00#  halafu chagua, ‘Vifurushi vya intaneti.”



No comments: