Mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Tanzania Samweli Sitta wawasili.


sitaa

Askari wakiwa wamebeba jeneza liliobeba mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Hayati, Samwel Sitta wakipita mbele ya Askari maalum kwa ajili ya kutoa heshima na baadaye kupakia jeneza hilo tayari kwa safari ya kuelekea nyumbani kwa marehemu leo Jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………….
Na: Frank Shija, MAELEZO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu amewaonga watanzania katka mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Tanzania marehemu Samwel Sitta aliyefariki dunia saa 10.00 usiku wa kuamkia tarehe 7 Novemba huko nchini Ujerumani alikokuwa kwa matibabu.
Mama Samia aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa 8: 44 mchana akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali tayari kwa kuupokea mwili wa marehemu Sitta uliowasili uwanjani hapo kwa usafiri wa ndege ya Emirate majira ya saa 9: 05 Alasiri.
Viongozi waliombatana na Mhe. Makamu wa Rais ni pamoja na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Idd, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Jumiya ya Afrika Mashariki Balozi Mahiga, Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angerah Kahiruki, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
Wengine ni Katibu Mkuu Kingozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda,na baadhi ya viongozi wa kiasiasa akiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Phillip Mangula, Msemaji wa Chama cha Mapinduzi Christopher Ole Sendeka,aliyekuwa Mbunge wa Tabora mjini Ismail Aden Ragge, Mzee Pius Msekwa na Profesa Ibrahim Aruna Lipumba wa CUF.
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo Waziri Mahiga alisema kuwa Taifa limepoteza kiongozi muhimu ambaye alikuwa na mahusiano mazuri na watu wa makundi yote kitu kilichomfanya kuwa mfano wa kuigwa.
Balozi Mahiga aliongeza kuwa kitu muhimu ambacho viongozi tuapaswa kujifunza kutuka kwake ni kuwa kiongozi siyo kipaji pekee bali ni ridhaa kutoka kwa watu kitu ambacho ndicho kilimfanya Sitta kuwa kiongozi katika katika nafasi mbalimbali za ungozi tokea Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne .
Aliongeza kuwa ameacha funzo kuwa ili uwe kiongozi imara atupaswi kukata taama badala yake unapaswa kusimamia misingi ya haki na ukweli ikibidi kutofautina na wenzako kwa maslahi ya taifa.
Kwa upande wake Msemaji wa CCM amemuelezea Sitta kama kiongozi aliyekuwa anahitaji sana katika kipindi kwa kuwa alijipambanua kama mpambanaji wa adui rushwa na ufisadi.
“ Tumempoteza mapambanaji muhimu has tukizingatia kuwa Serikali ya awamu hii chini ya AMIRI Jeshi Mkuu Mhe. Rasi Dkt. Magufuli ipo katika vita kubwa dhidi ya rushwa na ufisadi jambo ambalo Sitta alikuwa muumini wake” Alisema Ole Sendeka.
Utaritibu wa kuuga Mwili wa Marehemu Samweli Sitta zitaanzia na misaa ya shukrani nyumbani kwake hapo kesho(leo) saa 1:30 asubuhi baadaye utawasili katika viwanjwa vya Karimjee kwa ajili ya kuagwa kitaifa kuanzia 2;30 asubuhi kabla ya kuelekea Dodoma ambapo wabunge watapata fursa ya kumuaga kasha utaelekea Urambo moani Tabaro ambapo mazishi yake yanatarjiwa kufanyika huko siku ya Jumamsoi. Bwan ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.