Picha 12 kutoka Viwanja vya karemjee muda huu kuaga mwili wa Spika Mstaafu Samweli Sitta


Mwili wa aliyekuwa spika wa Bunge la Sita la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Marehemu SAMWELI SITTA umeagwa rasmi leo Jijini Dar es salaam katiika viwanja vya Karimjee na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli pamoja na viongozi wakuu wa serikali.ambapo mwili huo kwa mujibu wa ratiba utawasili Mjini Dodoma kwa ajili ya kuwapa nafasi wabunge wa Bunge la Tanzania kutoa Heshima zao za mwisho kabla ya safari ya kuelekea Urambo kwa Mazishi.

Hapa kuna baadhi ya oicha za Tukio Nzima muda huu Katika Viwanja Hivyo za Viongozi mbalim,bali walioshiriki katika Msiba huo.

Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dr Jakaya Kikwete pamoja na Mkamu wa pili wa serikali ya mapinzuzi ya zanzibar Balozi Seif Alli Idd wakati wa shughuli ya kumuaga kiongozi huyo aliyeliongoza Bunge la Tanzania kwa mafanikio makubwa.Picha na EXAUD MTEI WA HABARI24 BLOG
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akishindwa kujizuia na kujikuta akimwaga machozi katika shughuli hiyo baada ya kueleza Jinsi Spika Sitta alivyomsaidia hasa katika Masomo yake ambapo amese kuwa amewahi kumlipia ada ya chuo na kumsaidia kumaliza masomo yake ambapo tangu hapo akawa mmoja kati ya wanafamilia ya Samweli Sitta,

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.