Sunday, November 20, 2016

SEMINA MAALUM JUU YA JITIHADA ZA IMAM HUSSEIN NA MASIH YESU KATIKA KUSIMAMISHA HAKI NA AMANI YA DUNIA,SHEIKH JALALA ATOA NENO

Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA  akizungumza na wanahabari mapema Leo Jijini Dar es salaam Nje ya ukumbi ambapo kunafanyika Semina maalum ya Kujadili Juhudi za IMAM HUSSEIN na MASIH YESU katika kudumisha haki na Amani ya dunia
Watanzania wametakiwa kuhakikisha kuwa wanadumisha umoja na Amani iliyopo nchini ikiwa ni pamoja na kutenda mambo mema ili kuwaenzi kwa vitendo Immam Husein na Masih YESU ambao walipambana duniani kuhakikisha kuwa wanasimamia haki katika Dunia kwa ujumla.

Wito huo umetolewa Leo Jijini Dar es salaam na Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA  wakati wa semina maalum kwa ajili ya kujadili kwa pamoja Jitihada za wawili hao katika kuleta Amani na utulivu pamoja na kuleta haki na usawa Duniani ambapo Jalala amesema kuwa watu hao ni mfano wa kuigwa kwa sasa hii ikiwa ni semina pia ya kuadhimisha Arobaini ya Mjukuu huyo wa mtume Mohamad (s.a.s)

Sheikh Jalala amesema kuwa Semina hiyo inalengo la kuweka ulinganisho kwa watu hao wawili ambao ni Imam Husein na Nabii Isaa ambaye ni Yesu ambao wote kwa pamoja walikuja Duniani kwa ajili ya kuleta mabadiliko kwenye Dunia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo Haki kwa watu wote,na kutetea wanyoonge na kufanya watu wapendane katika Jamii.


Semina Ikiendelea
Ameongeza kuwa ni wakati wa watanzania kuacha mambo mambo mabaya na kuanza kufanya matendo ya kiumpendaza mungu yakiwemo kupendana,kupinga dhuluma,na kutetea wanyonge ili kuhakikisha kuwa wanawaenzi viongozi hao wa Kidini waliopambana kwa ajili ya dunia.
Picha mbalimbali za semina Hiyo ---






No comments: