Wakati Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania akiweka wazi mbele ya wanahabari kuwa mchakato wa
Katiba mpya itabidi usubiri ili apate nafasi ya kuinyoosha nchi kwanza,nao
Jukwaa la katiba Tanzania JUKATA wameibuka na kusema kuwa njia pekee ya
kuinyoosha nchi ni kuwa na katiba mpya na sio vinginevyo.
Kauli hiyo ya jukwaa la
katiba imekuja huku kukiwa na sintofaamu kuhusu kupatikana ama kutokupatikana
kwa katiba mpya mchakato ambao ulisimama na kupisha uchaguzi mkuu mwaka 2015 na
kuacha katika hatua ya Katiba Pendekezwa.
Akizungumza na
wanahabari leo Jijini Dar es salaam Mratibu wa jukwaa la katiba Tanzania Ndugu
Hebron Mwakagenda amesema kuwa wameshtushwa na kauli ya serikali ya Tano kuwa
mchakato wa Katiba mpya sio kipaumbele cha serikali ilihali katika Ilani ya
chama cha mapinduzi ndio Ilikuwa moja ya ahadi zao za kuhakikisha kuwa katiba
hiyo inapatikana.
“Tunampongeza Rais wa Tanzania
Mh Dkt Magufuli kwa juhudi kubwa anazozifanya kuirejesha nchi nmahala
inapostahili na JUKATA tunaamini kuwa katiba ndiyo chombo pekee ambacho
kitamsaidia Rais Kuirudisha nchi kwenye Mstari unaostahili,katiba pia itafanya
Rais magufuli aache Kumbukumbu ya kudumu ndani ya mioyo ya vichwa vya
watanzania kwa miaka mingi ijayo”amesema Mwakagenda ambaye ni mratibu wa
JUKATA.
Mratibu wa JUKATA Ndugu Hebroni Mwakagenda akizungumza na wanahabari leo. |
Aidha JUKATA wamesema
kuwa Duniani kote katiba ndiyo waraka unaowezesha wananchi kujitambua kama Taifa,pia katiba ni
waraka wa kiutawala unaoelezea bayana mgawanyo,madaraka,na majukumu ya vyombo
mbalimbali vya dola katika nchi hivyo katiba ndio waraka mama wa kisheria
unaoongoza shughuli zote za nchi na ni chimbuko la kisheria zote katika nchi,Hivyo
kauli kuwa huu ni muda wa kuinyoosha nchi bila kuwa na katiba imara ni jambo la
kupingwa wanaitaka serikali kurejesha mchakato wa katiba mapema.
Pamoja na hayo Jukata
kwa kuonyesha kuwa huu ndio muda muafaka wa Kurejesha mchakato wa katiba nchini
wamezindua kitabu maalum ambacho kinawahamashisha wananchi kuelewa mchakato huo
ulipofikia na nini kifanyike ili kuweza kuipata katiba mpya kwa sasa.
No comments:
Post a Comment