Sheikh Hemed Jalala--Tumuenzi Mtume Muhammad s.a.w. kwa kuwa na huruma kwa watu wote

Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia
ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh 
HEMED
JALALA wa pili kutoka kutoka kushoto akiongoza matembezi ya amani yaliyokuwa na lengo la kuadhimisha kifo cha Kiongozi wa waislam Mtume 
Mtume Muhammad s.a.w.
Picha na Exaud Mtei
Waislam wa Thehebu la Shia Ishnasheriya leo wamefanya maandamano ya Amani Jijini Dar e salaam maaandamano yaliyokuwa na lengo la kuadhimisha kifo cha kiongozi wao Mtume 
Mtume Muhammad s.a.w. ikiwa ni hatua ya kuadhimisha mambo mazuri aliyoacha duniani kiongozi huyo huku ikiwa ni Zaidi ya Miaka 1400 iliyopita tangu kifo chake.

Maandamano hayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa dhehebu hilo.


Akizungumza na wanahabari wakati wa maandano hayo ya Amani Jijini Dar es salaam Sheikh Jalala amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w. ambaye wanaadhimisha kifo chake ni kiongozi ambaye alitenda haki kwa watu wote na kuwa na huruma kwa watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote hivyo ni jukumu la wanadamu hususani watanzania kujifunza kuishi kwa Amani na upendo Bila kubaguana .
Sheikh Jalala amesema kuwa lengo kuu la matembezi hayo ambayo yameanzia Boma Jijini Dar es salaam Hadi Kigogo ni kuwaonyesha watanzania kuwa kuna haja ya kuwa na huruma ambayo alikuwa nayo Mtume Huyo ambayo ilimfanya kuwapenda wanadamu wote wakiwemo waislam na wakristo na kukaa nao meza moja bila kujali Imani zao,ambapo amesema watanzania tunatakiwa kuwa na Roho hiyo ili kudumisha Amani iliyopo.

Aidha katika hatua nyingine Sheikh Hemed Jalala ametoa wito kwa viongozi wa dini ya kiislam wakiwemo Masheikh,Maimam kuiga huruma ya Mtume Muhammad s.a.w. kwa kukaa na wachungaji,maaskofu,mapadre,na viongozi wa dini mbalimbali Tofauti na zao kwa lengo la kujenga umoja na mshikamano kama wanadamu.


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.