Friday, November 18, 2016

Tigo, Ebony FM kushirikiana uzinduzi tamasha la Mtikisiko mikoa ya Kusini

Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa matamasha ya Mtikisiko yanayolenga kunyanyua sekta ya muziki yatakayofanyika katika mikoa katika mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya kwa uratibu wa radio ya Ebony FM
Iringa, Novemba 17,  2016-Kampuni inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imesaini rasmi  uzinduzi wa tamasha la mwaka la Mtikisiko  kwa kushirikiana na kituo cha redio cha Ebony FM ambacho kina wasikilizaji wengi  katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Mtiririko wa matamasha hayo ya mwaka unatarajiwa kuanza Novemba 19 hadi 26  katika mikoa ya Njombe  na Mbeya kwa pamoja  ambapo onesho la fainali  litafanyika Desemba 10, 2016 mkoani Iringa.

Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha hilo mkoani Iringa, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya  Kusini Jackson Kiswaga alisema, “Tigo kila mara  inakuwa mstari wa mbele  katika kuhakikisha  kwamba vipaji vinavyoibukia katika sekta ya muziki  vinapewa jukwaa la kuonesha vipaji vyao na wasanii maarufu wanaweza kuunganishwa na mashabiki wao.

Tamasha la Mtikisiko  linakuja baada ya kumalizika kwa Tamasha la Tigo Fiesta 2016 hivi karibuni  ambalo Tigo ilikuwa mdhamini mkuu. Kiswaga aliwaaambia waandishi wa habari kwamba mashabiki watarajie ubora ule ule wa  burudani  waliouzoea  wakati wa tamasha la Fiesta.

Kushiriki kwa Tigo kutakwenda sambamba na  kuhakikisha  wateja wa Tigo na wale ambao sio wateja  wanafahamu na kuzielewa  huduma za Tigo wakati wa tamasha.
“Katika  kukuza uzoefu wa mteja na mtumiaji  wakati wa tamasha, tunatarajia wateja wetu  kutumia vilivyo kuanzishwa kwa huduma ya 4G LTE, Tiogo Pesa  na bidhaa na huduma nyingine zinazotolewa,” alisema Kiswaga.
Kiswaga alitangaza kuwa washiriki wa tamasha hilo kwa mwaka huu  watakuwa na nafasi ya kuchagua  njia ya kupata tiketi zao  kupitia Tigo Pesa  bila gharama ya ziada.

 Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo  washiriki wote wa tamasha  ambao watanunua tiketi zao  kupitia Tigo Pesa  watafurahia faida kwa kupata [punguzo la asilimia kumi  kwa kila tiketi itakayonunuliwa
Kiswaga alifafanua, “Kununua tiketi kupitia Tigo Pesa, wateja  kutoka mtandao wowote watapiga namba ya Mfumo wa Kifedha wa Simu (mfano *150*01# kwa Tigo), halafu chagua, “tuma pesa”, ikifuatiwa na chagua, “Mitandao Mingine” halafu chagua, “Tigo Pesa” na mwisho ingiza namba 0674444444.   

 Kwa upande wake mratibu wa Tamasha la Mtikisiko 2016, Austine Nyondo alisema, “Ninapenda kuchukua nafasi hii kuwaashukuru Tigo wakiwa ni wadhamini wakuu wa tamasha hili; mashabiki wetuwatarajie kupata burudani kutoka kwa wasanii maarufu katika  sekta ya  muziki.”
Aliarifu kuwa wakati wa tukio hilo  watasambaza vipeperushi kwa vijana  ambavyo vitakuwa na ujumbe  unaohusu Virusi Vya Ukimwi (VVU) kutokana na sababu kwamba mikoa  ya kusini inachukuliwa kuwa ni  “ukanda ulioathiriwa” na janga hilo.

Tamasha maarufu la Mtikisiko ambalo awali lilijulikana “Together Time”  lilibadilishwa jina mwaka 2008  lilianza mwaka 2007 na limeendelea kukua  katika kipindi chote cha miaka hiyo  na kupata umaarufu  kama tamasha la burudani la mwisho wa mwaka  katika mikoa ya kusini.

No comments: