Saturday, February 25, 2017

Itel Mobile yatoa msaada wa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi kutoka familia zenye kipato kidogo Arusha

Wakifurahia zawadi zao


                    Wanafunzi baada ya kupokea zawadi zao


Wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru jijini  Arusha wakitumbuiza kabla ya kupewa vifaa vya kujifunzia


Wanafunzi wakifurahia zawadi zao


                         Wanafunzi wakiwa na zawadi zao


Mwalimu Mkuu Bi. Rajab akipokea zawadi  toka kwa Steven Chen

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Uhuru  Bi. Rajabu akitoa shukrani kwa kampuni ya itel

Mwanafuzi akitoa shukrani kwa niaba  ya wenzie.


Meneja mauzo (T-shirt nyekundu katikati)  Steven Chen

Kampuni ya simu za mkononi ya itel, leo imetoa msaada wa vifaa vya masomo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru iliyopo jijini Arusha.

Akikabidhi msaada huo,  afisa mauzo wa itel kanda ya kaskazini Bwana Steven Chen amesema kampuni hiyo imeona ni jambo jema kusaidia wanafunzi wanaotoka familia zenye kipato cha chini kutokana na ukweli kuwa wapo wanafunzi wenye uwezo mkubwa darasani lakini kikwazo chao huwa ni umaskini.Kitu ambacho husababisha kukosa baadhi ya mahitaji muhimu kwaajili ya masomo kama vile daftari na vifaa vingine kwaajili ya kujifunzia.

“Sisi itel tunatamani kuwasaidia wanafunzi wote ambao familia zao hazina uwezo kiuchumi na wana malengo ya kufika mbali kielimu na kwa bahati mbaya wengine wanaishi na ulemavu.
Tunawaalika pia wateja wetuna wadau wote kwa ujumla kuweza kutoa misaada yao ili kuhakikisha watoto kama hawa wanaishi kwa furaha na kutimiza ndoto zao.” Alisema bwana Chen.
Chen aliongeza kuwa, sisi itel tunaamini tukiongeza jitihada zetu tunaweza kusaidia watoto wengi zaidi na kuwapa upendo na furaha na kujenga Dunia hii kuwa mahali salama penye upendo na amani. Kwa Pamoja Tunaweza!”

Katika utoaji wa msaada huo, vifaa mbalimbali viligawiwa kwa  wanafunzi takribani 45 ambavyo ni pamoja na mabegi ya shule, kalamu, penseli,madaftari, rula, mikebe na vingine.


Kwa upande wa uongozi wa shule ya Msingi Uhuru wameishukuru kampuni ya simu ya itel kwa msaada wa vifaa hivyo kwa wanafunzi. Akitoa shukrani kwa niaba ya uongozi wa shule hiyo, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Uhuru, Bi. Rajabu ameziomba  kampuni nyingine kuiga mfano wa kampuni ya itel, kwani kusaidia watoto wa namna hii kutafanya Tanzania kufuta ujinga na kufanya kuwa Taifa la watu wasomi.

Kwa upande wao wanafunzi wameishukuru kampuni ya itel kwa msaada wa vifaa vya kujifunzia kutokana na wao kuwa na uhitaji mkubwa.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzie, amesema wanashukuru kwa vifaa walivyopatiwa na kuongeza kuwa hii isiwe mwisho kwani wanaendelea kuhitaji zaidi.
Insert picture.

KUHUSU KAMPUNI YA itel
itel Mobile ni kampuni ya simu ambayo mpaka sasa ina umri wa miaka 10, ni kampuni ya masuala ya teknolojia na uvumbuzi, iliyojikita kwenye masuala ya SIMU. Karibu kipindi cha muongo mmoja kampuni hii imekuwa ikitamba kwa kusambaza bidhaa zake kwenye zaidi ya nchi 45 Duniani kote. 

Mwaka 2016, itel iliuza zaidi ya bidhaa zake milioni 50 barani Afrika na kuongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye tatu bora ya Kampuni za simu zenye idadi kubwa ya mauzo ya bidhaa zake.

Kila unaponunua simu ya itel, unapewa miezi 12 ya kuhudumiwa bure pale simu yako inapopata hitilafu yoyote ya kiufundi, hii ni kutokana na kuwa na vituo vya huduma kwa wateja wake baada ya mauzo yaani CarlCare service centers vilivyoko nchini.


No comments: