Saturday, February 25, 2017

TECNO L9+ MKOMBOZI WA WATANZANIA.


 


Kampuni ya simu yenye asili ya China, Tecno Mobile imekuja na ufumbuzi wa tatzo la simu janja (smart phone) kutokaa na chaji kwa muda mrefu.
Tecno wanajulikana kwa kua na simu zinazokaa na chaji kwa muda mrefu lakini zikiwa na ubora mkubwa, inatazamiwa hivi karibuni Tecno wataingiza sokoni simu  itakayokua mkombozi wa watanzania,  simu hii inatoka kwenye mfululizo wa matoleo ya L, ikitanguliwa na L8/l8 plus hii inakuja ni L9 plus .

Tecno L9 plus  inatarajiwa na kua betri lenye uwezo mkubwa Zaidi simu zilizoko sokoni  za aina yake, ikiwa ni 5000 mAh, kwa ukubwa wa betri hili pamoja na matumizi makubwa kusikiliza au kuangalia video, kupiga picha na kutumia mitandao ya kijamii   simu hii inaweza kufika masaa 72 ambayo ni sawa siku tatu ndipo mtumiaji anaweza kuchaji tena.

Pia Tecno L9 plus  pamoja na kua betri kubwa inakuja ikiwa na uwezo mkubwa kuchaji haraka, mtumiaji akichaji kwa muda wa dakika tano anaweza kuitumia simu kwa kupiga picha Zaidi ya 1000.

Kwa watanzania walioko mikoani simu hii inawafaa Zaidi hasa ukizingatia matatizo ya umeme kukatika katika kwa muda usio julikana, pia kupunguza kadhia  ya kutembea na vibeba umeme, power bank.

Tecno L9 plus  inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni pia ina usalama wa alama ya vidole maarufu kama finger print hali kadhalika   wemba wemba mzuri utakao mpa mtumiaji urahisi wa kuitumia.

Inatabiriwa kufanya vizur sokoni na wataalamu wa vifaa vya mawasiliano, Tecno L9 plus inasubiriwa kwa hamu  na watanzania wengi.



No comments: