Jumia Travel yazindua kampeni kwa ajili ya ‘Valentine’

Na Jumia Travel Tanzania

Ni takribani wiki moja imebaki kabla ya maadhimisho ya siku ya wapendanao duniani au ‘Valentine’s Day’ kama inavyojulikana na wengi. Katika kusindikiza shamrashamra za siku hiyo, Jumia Travel itawazawadia wateja chakula cha usiku kwa ajili ya watu wawili katika hoteli ya kifahari.


Akizungumzia juu ya kampeni hiyo, Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania, Bi. Fatema Dharsee amesema kuwa, “Katika kipindi hiki cha msimu wa wapendanao au ‘Valentine’, kama kawaida yetu Jumia Travel tumewaletea watanzania ofa ya punguzo kubwa la bei kwa hoteli mbalimbali nchini. Kampeni yetu imeanza tarehe 6 na itaendelea hadi tarehe 12 mwezi Februari, ambapo tumetoa punguzo la 50% katika huduma za hoteli zenye hadhi tofauti. Wateja watatakiwa kutumia nenosiri liendalo kwa jina la ‘LOVE50’ katika malipo yote ya huduma watakayoyafanya kwenye hoteli watakazozichagua.”


Zaidi ya hayo, katika kipindi hiki wateja watakaotumia mtandao wetu kujipatia huduma za hoteli, watakuwa na nafasi ya kuzawadiwa chakula cha usiku kwa ajili ya watu wawili kwenye hoteli ya kifahari. Lakini, ili kujishindia fursa hiyo itakubidi uitumie huduma hii kabla ya tarehe 10 Februari na hatimaye utakuwa umeingia kwenye kinyang’anyiro cha kuibuka mshindi” amesisitiza Bi. Dharsee.

Kampeni hii imelenga kuwapatia urahisi watanzania katika kufanya maandalizi na kupunguza gharama za kusherehekea siku ya wapendanao. Ifikapo siku hiyo watoa huduma wengi sehemu mbalimbali hupandisha gharama kutokana na uhitaji huwa ni mkubwa. Mbali na hilo pia hii inarahisha kujipanga mapema na kisha kuendelea na shughuli zako nyingine huku ukiwa huna wasiwasi na siku hiyo muhimu kwa wapendwa wako. Pia hii inatoa fursa kwa wateja kwenda kupumzika au kupata huduma kwenye hoteli ambazo walikuwa wanazitamani lakini wanashindwa kwenda kutokana na bei kuwa ya juu katika siku za kawaida.


“Tunafahamu kuwa shughuli ni nyingi na watu hawana muda wa kuanza kutafuta hoteli au kupatana bei za hoteli. Hivyo sisi kazi yetu kubwa ni kuwaondolea huo usumbufu na kuwarahisishia kila kitu. Natumaini wengi mtaifurahia ofa hii na tunawaahidi kuwaletea nyinginezo kadha wa kadha,” alihitimisha Meneja huyo Mkaazi wa  Jumia Travel Tanzania.
 
Mpaka hivi sasa, wateja wakitembelea mtandao wa Jumia Travel watajionea ofa kutoka hoteli kama vile: Hotel White Sands: Ledger Plaza Bahari Beach Hotel, Jangwani Sea Breeze Resort, Harbour View Suites, The Beach Resort, Golden Tulip Hotel, Ramada Resort, Mermaids Cove Beach Resort & Spa, Paradise Beach Resort, Golden Tulip Zanzibar Boutique Hotel, Nashera Hotel, Kwetu Hotel na Ngare Sero Mountain Lodge

Mbali na mtandao wa kampuni hiyo pia mteja anaweza kupata taarifa mbalimbali kwa kupita kurasa rasmi za mitandao yake ya kijamii ya Facebook (Jumia Travel), Twitter (@jumiatraveltz) na Instagram (jumiatraveltz).

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.