Monday, February 20, 2017

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ATANGAZA VITA NA WAVUVI HARAMU


Mkuu wa wilaya ya kinondoni,Ally Hapi ametangaza vita kwa watu wote wajihusisha na uvuvi haramu Ndani ya wilaya yake,baada ya kufanikiwa kumata nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya milioni 60.

Hapi ametangaza oparesheni hiyo Leo wakati alipokuwa kwenye ziara ya siku kumi katika Kata zote zilizopo kwenye wilaya yake yenye lengo ya kukagua shughuri mbali mbali za maendeleo.

Amesema ameshtushwa na kasi ya vitendo vya uvuvi haramu vinavyofanyika katika pwani ya bahari ya pweni jambo analodai linachangia kupotea kwa masalia ya samaki katika bahari huku akisititiza hatalifumbia macho suala hilo.
Amesema oparesheni hiyo imetokana na agizo alilotoa,Makamu wa Rais,Samia Suluhu alipokuwa mkoani mwanza alipokuwa akitangaza vita ya madawa ya kulevya pia alitangaza vita na watu wanaojihusisha na uvuvi haramu.
Amesema kwa sasa amemkabidhi kamanda wa 
Polisi wa kinondoni,Suzan Kaganda majina ya watu wanajihusisha na vitendo vya uvuvi haramu ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Pia amesema katika orodha hiyo ya majina ya wavuvi haramu Wapo watu wawili ambao ni viongozi wanaofanya shughuri ya uvuvi haramu,ambapo majina yao yamebainika baada ya kutajwa na wananchi.
Naye afisa Uvuvi wa Wilaya hiyo Grace Katama amesema kwa kipindi cha toka mwezi semptemba mwaka Jana hadi February mwaka huu wamefanikiwa kukamata nyavu za uvuvi haramu zenye thamani ya milioni 60
Huku pia wamewakamata watu saba wanajihushisha na uvuvi kwa kutumia
mabomu,

Pia amesibitisha kufunguliwa kesi moja ya wavuvi katika kituo cha Polisi Ostarbey ambao walinusurika kufa kutokana na wavuvi wenzao kutumia Bomu wakati wa uvuvi,baada ya Bomu hilo kuwajeruhi.
Katika hatua nyingine ,Hapi amewaagiza watendaji wote wa kata mbali mbali kuhakikisha wanalinda maeneo yote ya wazi yaliyopo katika maeneo  yao,ili yasivamiwe na watu kwenye fedha.
Mkuu huyo wilaya katika ziara yake hiyo ya siku ya kwanza ametembelea shule mbali ,vituo vya polisi vinavyojengwa pamoja nyumba za walimu ili kukagua Ujenzi wake,Huku akiwataka wananchi kujitokeza kuja kutoa kero mbali mbali zinazowakabili katika maeneo yao ili ziweze kufanyiwa ufumbuzi.

No comments: