![](http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/3256744/medRes/1359057/-/itksjt/-/pic+mwanaume.jpg)
Katika Kipindi cha E Sport Kutoka radio eFM kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Kamanda SIMON SIRRO amemdhibitishia Mtangazaji Maulid Kitenge kuwa Vipimo vya mkemia mkuu wa serikali alivyofanyiwa Tajiri huyo vinaonyesha kuwa ni Mtumiaji wa Madawa ya kulevya(Hakuyataja aina yake) na kusisitiza kuwa kesho mtuhumiwa huyo atapandishiwa kizimbani kujibu shitaka hilo.
Akielezea afya yake tangu alazwe Hospitali Juzi amesema kuwa mwenyekiti huyo wa yanga yuko VIzuri na sasa ameruhusiwa Kutoka Hospitalini na kurejeshwa Mahabusu polisi kusubiri kupandishwa Kizimbani hapo kesho.
Sirro amesema kuwa Habari kamili kuhusu sakata hilo na watuhumiwa wengine wakiwemo wasanii waliokamatwa zitatolewa kesho mbele ya wanahabari Jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment