![](http://allafrica.com/download/pic/main/main/csiid/00360249:7715ac8cf414dfa5d61b29f6718daf6d:arc614x376:w1200.png)
Kesho Alhamisi Februari 16, 2017 timu za mpira wa miguu za Simba
na African Lyon zitacheza mechi yao katika Raundi ya Sita ya kuwania Kombe la
Shirikisho la Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup.
Mchezo huo awali ulipangwa kufanyika Machi mosi, 2017 lakini
ulirudishwa nyuma kwa sababu za kiufundi kutoka timu zote mbili.
Michuano ya raundi hiyo ya sita, itaendelea tena Februari 24,
mwaka huu kwa michezo minne kuchezwa kwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni
kasoro mchezo mmoja tu utakaochezwa saa 1.00 jioni.
Michezo ya siku hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya
Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa
Kaitaba mjini Bukoba.
Mechi nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma
na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea
ilihali Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika
saa 1.00 usiku.
Jumapili Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na
Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania
Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini
Mbeya.
Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment