![](http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2882290/medRes/1126929/-/olyi9hz/-/pic+nkongo.jpg)
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF), waamuzi hao ni Alex Muhabi Nsulumbi atakapuliza filimbi uwanjani.
Nsulumbi atasaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati
Mwamuzi wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika
Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.
Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama
ambavyo Young Africans walithibitisha CAF majuma mawili yaliyopita kabla ya terehe
ya mchezo huo ambayo ni Februari 18, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment