TECNO MOBILE YASHINDA KAMPENI BORAKampuni  inayoongoza kwa mauzo ya simu nchini Tanzania, TECNO MOBILE imefanikiwa  kushinda tuzo za  Tanzania leadership Awards  zilizofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es salaam. 

Katika mchakato wa tuzo hizo zilizoandaliwa na Purple  cow media Tecno   iliingia katika tatu bora ikiwa inashindana na kampuni mbili kubwa nchini Tanzania, kampuni ya mawasiliano ya simu TIGO na kampuni ya vinywaji  TBL , zote zikiwa katika  kitengo cha kampeni bora MITANDAO YA Kijamii ya  mwaka katika mitandao ya kijamii.
Tecno waliingia katika kinyang’anyiro kupitia kampeni yao ya simu  maarufu ya TECNO  CAMON  C9, katika kampeni iliyoshika hisia za  watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii kutokana na kuwapa nafasi watumiaji  wa simu kupiga picha kutokana na  maelekezo yaliyokua yanatolewa na account za mitandao ya kijamii  za kampuni,  washiriki washindi walipewa  zawadi  za aina mbalimbali   zikiwemo simu za TECNO CAMON C9.


 Tecno imekua kampuni ya kwanza ya simu kushinda katika kategori hiyo ya kampeni bora ya mwaka ya  mitandao ya kijamii kutokana na uwezo wake mkubwa uliojidhihirisha kwa kuwapa nafasi kubwa watumiaji wa mitandao na wateja wake kufikisha matzo yao na kusaidiwa lakini pia wateja kuongea na watu mbalimballi maarufu kama Salma Jabir, Hamisa Mobeto pamoja na Idriss Sultani huku zawadi kemkem zikitolewa kwenda kwa watumiaji wa mitandao waliofwata TECNO mobile katika mitandao.

Jamii ya Kitanzania itaendelea  kufaidika na mitandao ya kijamii kupitia kampuni kubwa ya  Tecno Mobile wakifanya matukio mbalimbali ikiwemo kampeni mpya  iliyopata umaarufu ya KAMA MBELE washindi wakipata nafasi ya kwenda kushudia mchezo wa mpira wa miguu katika jiji la Manchester wakiwa na mchekeshaji Idris Sultan, pamoja na Kampeni UPENDO inayowataka watumiaji kuweka picha au video mitandao wakisema upendo kwao ni nini na video/picha bora itampa nafasi mshiriki kuchaguliwa kwenda kusheherekea siku ya wapendao katika hotel kubwa Nchini. About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.