Monday, February 6, 2017

UJUMBE WA MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM KWENDA KWA WAZAZI

MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ,amewataka wazazi wa jijini hapa kuhakikisha kwamba wanashirikiana kikamilifu na bodi za shule ili kuleta mabadiliko ya matokeo ya wanafunzi wanao maliza masomo yao.


Aidha amewataka wazazi kuwaweka watoto wao kwenye misingi mizuri ya kimaadili ikiwemo kutumia mitandao, simu za mkononi kwakuwa nijambo linalofanya watoto kufanya vibaya kwenye mitihani yao.


Meya Isaya alitoa kauli hiyo jijini hapa mwishoni mwa wiki aliposhiriki ibada na waumini wakanisa la Ufufuo lililopo Kimara Bonyokwa jijini hapa ambapo pamoja na mambo mengine alisema kwamba suala la matokeo mabovu yaliyopatikana katika jiji linaweza kuhusisha na mambo ya mitandano kutokana na kwamba watoto wengi sikuhizi wanatumia muda mwingi kwenye mitandao badala masomo.

Alisema suala la mitandao kwakisi kikubwa kimefanya jiji la Dar es Salaam kupata  matokeo hayo, kwakuwa wazazi wameruhusu watoto wao kutumia simu ambazo zinajihusisha na mambo ya mitandao.
“ Hivi sasa kila mwanafunzi anatumia simu za smati ambazo zinamitandao ya Watasp, Istragram, Tango, Facebook, na mambo mengine , sasa muda mwingi sana wanaingia kwenye mitandao kwa ajili ajili ya kuwasiliana kwa njia ya mitandao badala ya kusoma, na wazazi wanawaangalia , nawao ndio wanawanunulia hizo simu, kwakweli jambo hilo kama wazazi hawatabadilika inadidi iwekwe sheria ya kudhibiti jambo hilo” alisema Meya Isaya.

Alisema kwamba walimu shuleni wasihofie kuwakemea watoto, kuwanyang’anya simu wanafunzi pindi wanapowaona wanatakiwa kuweka mkazi kwa wanafunzi ambao wanatumiasimu za mko
Aliongeza kwamba , kila mzazi anatakiwa kushirikiana na bodi za shule,kwa kila eneo waliopo ili kushirikiana kikamilifu katika kuweka mipango endelevu ya kuwasaidia watoto katika suala zima la elimu badala ya kusubiri serikali kufanya kila jambo.

Alisema kuwepo kwa sera ya elimu bure isifanye wazazi washindwe kujihusisha kwenye michango ya kupeleka maendeeo badala yake wanatakiwa kushiriki kikamilifu kwenye maeneo ambayo wanahitajika.


“ Tuna sera yetu ya elimu ambayo ni ya elimu bure, jambo hili lisifanye wazazi kutumia serikali kila kitu, lazima tuige mifano kutoka kwa wenzetu wa Kenya, Uganda ukienda utaona wanavyoshirikiana na serikali vizuri, bila kujali kwamba jambo hili linatakiwa kufanywa na serikali” aliongeza. 

Hata hivyo katika hatua nyingine Meya Isaya amewaomba watanzania kuendelea kuiombea Nchi ya marekani na rais wake ili aweze kufanya mambo ambayo hayawezi kuathiri nchi nyingine.
 MWISHOO.


No comments: