SIASA

ACT WAZALENDO KUADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA KWA CHAMA HICHO

Maadhimisho ya Siku ya Kuzaliwa Chama cha ACT Wazalendo:

Tarehe 05 Mei 2017, Chama cha ACT Wazalendo kitatimiza miaka mitatu tangu kilipopata usajili wa kudumu tarehe 05 Mei 2014 wakati huo kikiitwa ACT Tanzania.

Maadhimisho ya miaka mitatu ya kuzaliwa kwa ACT Wazalendo yatafanyika Kahama Mjini Mkoani Shinyanga tarehe 05 Mei 2017.

Kwa kuzingatia falsafa ya Mpango Mkakati wa Chama ya Siasa ni Maendeleo, maadhimisho ya miaka mitatu ya Chama yatajumuisha shughuli mbalimbali za kijamii kama vile usafi kwenye masoko ya mji na hospitali na kuwatembelea wafungwa. Viongozi wa Chama wa kitaifa na mkoa wa Kahama watashiriki kwenye shughuli hizi.

Wanachama, wapenzi na wananchi kwa ujumla mnakaribishwa kwenye sherehe hizi za maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama chetu cha kizalendo.

Maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama yatafuatiwa na mafunzo ya siku mbili kwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama kuhusu Itikadi, Oganaizesheni na Usimamizi wa Rasilimali Fedha yatayofanyika tarehe 6 Mei hadi tarehe 7 Mei 2017.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.