Sunday, April 2, 2017

FNB KUTOZA GHARAMA MOJA KWA MIAMALA YA KIBENKI

 Mkuu wa Huduma za Rejareja wa First National Bank, Bw. Francois Botha (Kushoto) na Mkuu wa Matawi na za Huduma za kibenki, Bw. Kitumari Massawe (Kulia) wakishilia Bango wakati wa mkutano na waandishi wa habari kama ishara ya kuanzisha huduma ya kutoza gharama moja kwa miamala ya kibenki kwa wateja wake ambao wana akaunti ya Gold ya Hundi. (Picha: Mpiga Picha Wetu)
Mkuu wa Matawi na Huduma za Kibenki, Bw. Kitumari Massawe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya faida ya akaunti ya Gold ya Hundi ambapo wateja watalipa shillingi elfu kumi na sita kwa mwezi ambayo ni gharama moja na kuondoa adha na utaratibu wa kulipa huduma kwa muamala mmoja mmoja.( Kushoto) ni Mkuu wa Huduma za Rejareja wa Benki hiyo, Bw. Francois Botha na Meneja Masoko wa First National Bank, Bi. Blandina Mwachang’a (Kulia).
Mkuu wa Huduma za Rejareja wa First National Bank, Bw. Francois Botha ( Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, na kutangaza benki hiyo kuanza kutoza gharama moja kwa miamala mbalimbali kwa wateja wake ambao wanatumia akaunti ya Gold ya Hundi. ( Kushoto ) ni Mkuu wa Matawi na Huduma za kibenki wa First National Bank, Kitumari Massawe. --- First National Bank Tanzania imetangaza kuanza kutoza gharama moja kwa miamala mbalimbali kwa wateja wake ambao wana akaunti ya Gold ya hundi ikiwa ni mojawapo ya jitihada za benki hiyo kuwapa unafuu watumiaji wa huduma za kibenki. Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha amesema jijini Dar es salaam leo kwamba benki hiyo itawapatia wateja wake fursa ya kufanya miamala mbalimbali ya huduma za kibenki mara nyingi wawezavyo kwa gharama moja iliojumuishwa na bila kulipa gharama za ziada. “Wateja watalipa shilingi elfu kumi na sita tu kwa mwezi ambayo ni gharama moja, hii itaondoa adha na utaratibu wa kulipia huduma kwa muamala mmoja mmoja. Mpango huu unatarajiwa kuwanufaisha wateja wetu kwa kuwapunguzia gharama za miamala huku wakitumia fedha hizo kujiongezea akiba zaidi kwenye akaunti zao. Hatua hii ni ya faida kubwa kwa wateja wetu wa akaunti ya Gold ya hundi na wateja wengine kwa ujumla”. Mpango wa gharama moja kwa miamala utajumuisha utoaji wa fedha kwenye ATM yoyote, miamala ya TigoPesa, malipo ya bidhaa kama DSTV, LUKU na muda wa maongezi, kuweka maelezo ya kuhamisha fedha toka kwenye akaunti, kufanya manunuzi ya bidhaa kwa kutumia kadi katika vituo vya mauzo popote duniani, pamoja na kuweka fedha taslimu na hundi kwenye akaunti ikiwemo kwenye mpango huu.

No comments: