HABARI MPYA

MH BILAL AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA USONJI DUNIANI,TIZAMA HII

 Tarehe 2 ya mwezi wa 4 dunia nzima inaadhimisha siku ya usonji Duniani na kwa hapa nchini kwetu maadhimisho hayo yamefanyika katika shule ya al muntazir. Yakitanguliwa na matembezi yaliyoanzia shule ya Al Muntazir ya wavulana iliyopo karibuni na hospital ya aghakani  mpaka shule ya al muntazir ya wasichana kupitia barabara ya barack obama na kutokea barabara ya umoja wa mataifa.

Matembezi hayo yalikuwa na kauli mbiu inayosema kuwa “TUWAPENDE NA TUWALINDE” ikiwa na maana ya kuwapenda na kuwapatia ulinzi watoto wenye mahitaji maalumu.

Pia maandamano hayo yaliudhuriwa na Makamu wa Rais mstaafu Dr Mohamed Garib Bilal ambae pia alikuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo. DR Bilal alipongeza jitihada hizo zilizofanywa na uongozi wa shule hiyo kwani ni mfano wa kuigwa kwa jamii kwa kuwa leo hii imeweza kuwakutanisha watoto na wazazi toka sehemu mbalimbali lengo ni kuwapa elimu jinsi ya kuwalea watoto hawa.

Kuwa inafahamika kuwalea watoto hawa kunachangamoto nyingi lakini inabidi kuweza kizikabili kwa kuwa watoto hawa ni zawadi toka kwa mungu na mungu anapima utu wetu kupitia watoto hawa. Lakini pia sio kuwapenda na kuwatunza tu bali kuwaweka pamoja na jamii ili wao kuweza kujiona ni sehemu ya jamii na sio kutengwa kwani wanajiona wapweke.

Na hii ndio sababu iliyopelekea Khoja Shia Ithal Ashel Mamaat kupitia Centre Board of Education kuweza kuanzisha shule hizi kwa kuwa waliweza kuona changamoto hizi. Na kuamua kuanzisha shule hizi lengo ni kuwasaidia vijana hawa wenye mahitaji maalum mnamo mwaka 2013 na shule ikiwa inapokea watoto kuanzia miaka 3 mpaka miaka 22.

Lakini pia mgeni Rasmi DR. Bilal aliweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja taslimu alizo zitoa hapo akimkabidhi Mwenyekiti wa Khoja Shia Itha ashel Jamaat central board of education Mr Intiaz Lalji kwa kuweza kuongeza nguvu katika zoezi la kuwasaidia vijana hao. Huku akiwasilisha mchango Makamu wa Raisi wa sasa Mama Samia suluhu aliyeweza kutoa mchango wa million 5.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.