Mkurugenzi Mtendaji wa JUKATA Bwana Hebron Mwakagenda Pamoja na wadau mbalimbali wa Katiba nchini Tanzania wakizngumza na wanahabari Leo Jijini Dar es Salaam. |
Ikiwa ni siku kadhaa Tangu Serikali kupitia kwa waziri Mpya wa Katiba na Sheria Mh Palamagamba Kabudi Kutoa tamko Mjini Dodoma juu ya nia ya serikali kutaka kurejesha mchakato wa katiba mpya ili kumalizia mchalato huo ambao ulisimama kwa muda,Hatimaye Jukwaa la Katiba nchoni Tanzania JUKATA wameibuka na kuitaka serikali kuhakikisha kuwa mchakato huo unazingatia matakwa ya watanzania na uhalisia wa mchakato wenyewe.
Akizungumza na wanahabari Leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa JUKATA Bwana Hebron Mwakagenda Pamoja na Pongezi kwa waziri huyo kuteuliwa kushika nafasi hiyo nyeti JUKATA wamesema kuwa wanaamini kuwa sasa ni wakati muafaka wa kurejesha mchakato wa katiba kwani Waziri huyo pamoja na kuwa ni gwiji na mtaalam wa sheria na mambo ya katiba lakini pia ameshiriki kikamilifu katika mchalato huo akiwa kama Kamishna wa Tume ya mabadiliko ya katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba hivyo wanaamini atautendea haki mchakato huo.
Aidha wamemtaka Waziri huyo kuhakikisha kuwa katika Bunge hili la mwaka 2017 anapeleka miswada ya marekebisho ya sheria zinazosimamia mchakato huo ikiwa ni pamoja na sheria ya kuanisha ni hatua gani za kupita ili kufikia kupata katiba Mpya.
Aidha wameeleza kasikitiko yao kwa serikali kutotenga Fedha tena kwa mwaka wa pili kwa ajili ya kukamilisha mchakato huo ambao uliingia katika sintofahamau mapema mwaka juzi na hatimaye kusimamishwa kwa ajili ya kupisha uchaguzi.
No comments:
Post a Comment