Tuesday, April 4, 2017

Tigo yazindua kituo cha kwanza cha aina yake cha huduma kwa wateja

Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Diego Gutierrez  akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo kipya cha kisasa cha huduma kwa wateja jijini Dar Es Salaam mapema leo. Wengine pichani ni Meneja wa Ubora wa huduma kwa wateja, Mwangaza Matotola, Ofisa Mtendaji Mkuu wa PCCI Nidal Kamouni na Mkuu wa kitengo cha uendesheji wa huduma kwa wateja Tigo, Zaeem Khan.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa PCCI,Nidal Kamouni akiongea na wanahabari

Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Diego Gutierrez (kushoto)na Ofisa Mtendaji Mkuu wa PCCI Nidal Kamouni wakikata utepe kuzindua kituo kipya cha kisasa cha huduma kwa wateja cha Tigo jijini Dar Es Salaam mapema leo.

. Meneja wa Ubora wa huduma kwa wateja Tigo, Mwangaza Matotola akitoa maelezo ya jinsi ya uendeshaji wa kituo  kwa mkurugenzi mtendaji wa Tigo, Diego Gutierrez na wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kituo hicho kipya cha huduma kwa wateja cha Tigo.
Timu ya watoa huduma kwa wateja wakionyesha jinsi ya utendaji wa kazi zao
Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali leo imetangaza kufungua  kwa kituo kipya cha kisasa cha huduma kwa wateja (Call Centre) kikiwa ni cha kwanza nchini Tanzania.
 Ikiwa inajivunia teknolojia ya hivi karibuni kituo hicho cha miito  kimetengenezwa ili kuwapatia wateja wa Tigo huduma ya daraja la juu duniani katika namna ambayo ni ya ufanisi na uhakika  zaidi kutoka kwa mawakala wa huduma kwa wateja waliopata mafunzo ya hali ya juu.
 Kituo hicho kipo kitalu namba  395 Ursino   barabara ya Kawawa, Kinondoni jijini Dar es Salaam kikiwa kimesaidiwa Kundi la PCCI ambalo ni kiongozi wa soko katika  uzoefu wa mteja na uendeshaji wa vituo vya huduma.
 Akizungumza  kuhusu kituo kipya cha miito  ya simu wakati wa hafla ya kuashiria uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Diego Gutierrez alisema, “Uwekezaji wetu katika kituo hiki kipya cha miito ya simu kunaashiria kujituma kwetu katika kukua na kubadilisha mtiririko  ambao tumekuwa tukitumia kuwafikia wateja wetu. Washirika wetu wa kibiashara  na wateja binafsi hivi watarajie  kupata huduma ya hali ya juu kwa mteja inayopatikana hapa nchini, ikiwa inatolewa na  na mawakala wa kituo  walio tayari kutoa huduma bora.”
 Gutierrez alifafanua  kuwa kituo hicho kipya kimefungwa teknolojia ya aina yake  na miundombinu iliyo na usalama wa data  utakaowezesha  kulinda taarifa za wateja pamoja na utambulisho wao.
 Aliendelea kuongeza kuwa kituo hicho kinajumuisha chumba cha mafunzo ambapo watu binafsi wanapigwa msasa  ili kuwa mawakala wa kituo.
PCCI inaendesha shughuli zake katika maeneo 20 duniani  ikiwa na wafanyakazi 7,000 ambao watakisaidia kituo cha Tigo Tanznaia katika kutoa  jukwaa la kipekee  katika uzoefu wa kuhamasisha wateja na kuwa na ukaribu nao.  Ikiwa inajiweka katika mwenendo uliopo sasa  PCCI itawapatia wateja wa Tigo sio tu huduma ya kawaida ya  ya kuwasiliana na kituo  bali pia  suluhisho la  jipya la kidijitali la huduma kwa mteja ambalo linajumuisha mtandao wa jamii kuchati kielektroniki na barua pepe.
 “Tunafurahi kushirikiana na moja ya kampuni ya mawasiliano ya simu inayoongoza duniani, Tigo kama mshirika aliyechaguliwa kusimamia kituo chake cha mawasiliano nchini Tanzania. Uendeshaji wa kituo hiki kipya  unashirikisha wataalamu wa ndani wa PCCI na  na makao makuu yayake yapo Dubai. Kadhalika kama sehemu ya  ushirikiano huu PCCI itaajiri zaidi ya watu 500 ili kusaidia vipaji vya ndani, “ alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa PCCI Nidal kamouni.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Tigo uendeshaji wa huduma za wateja, Zaeem Khan  alithibitisha tena  kujikita kwa kampuni  hiyo ya mawasiliano ya  simu katika kutoa  teknolojia ya hali ya juu kwa wateja wake akibainisha kuwa kituo hicho kipya  kwa mara nyingine tena  kimeiweka Tigo katika nafasi ya kuongoza katika soko.
 “Tunapenda  kuwahakikishia wateja wetu kwamba kupitia kituo  miito  wataendelea kupokea  huduma za hali ya juu  zisizo na kasoro kuwa na mawasiliano ya ana kwa ana na kushikamana na kuliko hai  kutoka kwa timu zetu zilizopata mafunzo vizuri,” alisema Khan.
 Khan alifafanua  kwamba uwezo wa Tigo wa kujibadili  kulingana na mabadiliko ya mahitaji ya wateja  na matamanio yake  yameiweza kutoa kwa ufanisi mkubwa hatua kwa hatua  na hivyo kuifanya kusimama kivyake ndani ya soko.
 

Mwisho

No comments: