Saturday, April 29, 2017

LHRC WAKUTANISHA WADAU KUIJADILI REPORT YA CAG,HAYA NDIYO WALIYOZUNGUMZA

Mratibu wa Kituo cha sheria Na haki za Binadamu Nchini Tanzania (LHRC), Anna Henga akizungumza katika wakati wa  mkutano mfupi wa wadau mbali mbali wa kujadili ripoti ya CAG ya mwaka 2015-2016 ambayo iliyowasilishwa Bungeni hivi karibuni  mkutano  ulioandaliwa na  Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

MSOMI wa Masuala ya Uchumi nchini,Profesa  Honest Ngowi ameishauri serikali kuhakikisha wanatekeleza mapendekezo yaliyotolewa kwenye Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) katika  Ripoti yake ya Ukagauzi kwa mwaka wa fedha 2015-2016 ili kuweza kuisadia serikali kuondokana na changomoto zilizoibuliwa kwenye Ripoti hiyo.

Pia Msomi huyo amewatoa wasiwasi wananchi kuhusu ongezeko la deni la Taifa kwa kusema ni lazima serikali ikope fedha hizo ili ziweze  kupelekwa  kwenye miradi ya maendeleo.
Profesa Ngowi ambaye ni Mhadhiri wa Uchumi kutoka chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro ,ameyasema hayo wakati wa  mkutano mfupi wa wadau mbali mbali wa kujadili ripoti ya CAG ya mwaka 2015-2016 ambayo iliyowasilishwa Bungeni hivi karibuni ambapo mkutano huo  umeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Profesa Ngowe amesema ni vema serikali ikahakikishwa inayatatua mapendezeko ya mkaguzi huyo wa serikali.
“CAG ametoa mapendezeko mazuri ambayo serikali ikiyafanyia kazi tuweza kuinua uchumi kwani kuna mapendekezo ya kuhakikisha serikali inafuta misamaha ya kodi,watumishi hewa pamoja kuongeza watumishi wa umma kwenye maeneo ambayo hayana watumishi kabisa ikiwemo mkoa wa Ruvuma”amesema Profesa Ngowe.

Hata hivyo,Msomi huyo amesema kitendo cha deni la Taifa kuongezeka sio dhabi kama serikali inakopa fedha kwa kuziendeleza fedha hizo kwenye Miradi ya maendeleo huku akisisitiza serikali kuhakikisha wanalipunguza deni hilo.
“Nimeona makadilio ya Bajeti ya mwaka 2017-2018 serikali imetenga trioni 9 kwa kupunguza deni la Taifa naona hili ni jambo jema sana.”ameongeza kusema.

Kwa Upande wake Mratibu wa (LHRC), Anna Henga amesema katika mkutano huo wadau wameonyesha masikitiko kwa hatua ya CAG katika ripoti yake kuongezeka kwa misahama ya kodi ambayo wamedai misahama hiyo haina tija/.
“Wadau wameshangaa kweli leo makampuni makubwa ya madini yanapewa misamaha ya kodi huku mkulima hakikosa misahama hiyo kwa hili ni jambo kumuumiza kabisa mtanzania”amesema Bi Henga.




No comments: