Dar es Salaam Aprili 28, 2017- Kampuni inayoongoza Tanzania katika maisha ya kidijitali Tigo leo imetoa kompyuta 10 kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wasichana katika Tehama, tukio ambalo linachangia kuziba pengo la jinsia katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasialiano (Tehama). Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Ongeza Upeo, Badilisha Tabia”.
Siku ya Kimataifa ya Wasichanaktika Tehama ni mkakati wa Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano ya simu (ITU) ambao unalenga kuwezesha na kuwahimiza wasichana na wanawake vijana kuzipa nafasi ajira zilizopo katika sekta ya teknolojia ya habari.
Akizungumza wakati wa tukio la kutoa msaada huo lililofanyikakatika Shule ya Sekondari Jangwani, Ofisa Mkuu wa Ufundina Mawasiliano wa Tigo, Jerome Albou alisema kuwa Tigo imejikita katika kuchangia uwezeshwaji wa wanafunzi, hususani wasichana, ili waweze kuingia katika mtiririko wa ulimwengu katika habari na uelewa, ambapo watajifunza, na kupanua ubunifu wao na kushirikiana na wenzao kote duniani kupitia mikakati iliyo ndan ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
“Msaada wa kompyuta hizi upo katika mkakati wa Tigo wa kusaidia kuwawezesha wanawake na wasichana kupitia teknolojia za habari na mawasiliano,” alisema Albou akibainisha kuwa Tigo imejikita katika kutekeleza dira ya serikali ya kuibadilisha nchi kuwa ndani ya uchumi wa uelewa ifikapo mwaka 2025 kupitia ukuzaji na kuwavutia wanawake kuingia katika mafanikio makubwa ya nguvukazi anuai.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano, Dorosela Rugaiyama,aliipongeza Tigo kwa mchango huo, akisema kwamba kompyuta hizo zitawafikisha mbali wanafunzi katika kusambaza stadi na uelewa wa Tehama za kisasa kwa vijana, kuwawezesha kukabiliana na changamoto za mwenendo wa mabadiliko ya habari katika jamii na duniani kwa ujumla.
Shughuli nyingine ambazo zilifanyika katika Shule ya Sekondari Jangwani, ambayo ni mojawapo ya vituo vya miradi ya Shule-elektroniki ya Tigo tangu mwaka 2015, ni pamoja na uwasilishaji wa program mbalimbali za komputa kutoka kwa wanafunzi vijana ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao chini ya mkakati wa Kidijitali wa Waleta mabadiliko ya Tigo (Tigo Digital Changemakers-TDC)-wakisimamiwa na washindi wa zamani wa TDC, Carolyne Ekyarisiima, ambaye Mradi wake wa Apps and Girls unaziba pengo katika Tehama kupitia teknolojia za kidijtali, na Faraja Nyalandu muasisiwa Shule Direct, ambao ni ujasiriamali jamii kidijitali ambao unatoa mada za elimu katika kusaidia kukabiliana na changamoto za uhaba wa walimu.
Serikali ya Tanzania inazitaka shule kufundisha masomo ya msingi ya kompyuta lakini ni asilimia 5 tu ya shule zina kompyuta nchini kwa sasa. Umahiri katika Tehama unabakia kuwa mbali lakini kutokana na Tigo kutoa msaada pamoja na wadau kuchangia malengo ya mabadiliko yanaweza kuhamasisha wadau wengine kuchangia kufikiwa wa malengo yaliyowekwa na serikali yanayolenga katika kuziwezesha shule zaidi ya 700 na zana za Tehama zikiwemo kompyuta.
Mradi wa Shule-elektroniki ni moja ya miradi ya kampuni katika mikakati ya uekezaji kijamii na kupitia mradi huu Tigo imeweza kuunganisha shule zaidi ya 60 za serikali nchini Tanzania na intaneti ya kasi na ya uhakika ya 4G LTE.
No comments:
Post a Comment