Thursday, April 27, 2017

MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM GEUKA GUMZO HUKO IRAN TIZAMA PICHA AKIWA KWENYE MKUTANO NCHINI HUMO

Inline image 1
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwa akisikilia jambo wakati wa mkutano uliomalizika jana jijini Mashahad Nchini Iran , pembeni yake kulia mwenye baragashea ni Meya wa jiji la Acra Mohamed Sowah na wakwanza kushoto ni Meya wa jiji la Kamapa Elias Lukwag.

Inline image 2

Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wapili kulia akiwa kwenye mkutano jijini Mashad Nchini Iran,   wa kwanza kulia ni Meya wa Damascas  Nchi Syria Inline image 3

Inline image 4

Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwa kwenye mkutano jijini Mashad nchini Iran

NA MWANDISHI WETU,  Mashahad
 MEYA wa Jiji la  Dar es salaam Isaya Mwita amekuwa gumzo katika mkutano uliomalizika jana Jijini Mashahad Nchini Iran baada ya kusema kwamba Tanzania haina dini ila watu wake wana dini.
Meya ambaye yupo Nchini Iran kwa ziara ya kikazi ya siku 10, alijikuta kwenye gumzo hilo wakati akichangia mada iliyokuwa ikiendelea ndani ya mkutano huo ambao ulimalizika jana.
Meya alisema kwamba Tanzania ni Nchi ya amani ambayo haijawahi kuwa na ubaguzi wa rangi, dini wala kabila na kwamba kila mmoja aliyepo ndani ya nchi hiyo  anajivunia kuwa mtanzania.
Alisema hali hiyo imekuwa ni tofauti hata katika maeneo mengine kwani yapo mataifa ambayo hadi sasa yanajadili udini na ukabila , na kushauri kwamba ni vema viongozi wa kila majiji kujitahidi kutumia nafasi hiyo ili kuondokana na matabaka.
“ Watanzania kuna mambo ambayo tulijiwekea tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambapo ndio msingi mkuu tulionao, hakuna ubaguzi wa dini wala rangi, jambo kama hili ni maeneo machache sana katika Nchi zetu kuyakuta,hivyo Tanzania tunajivunia kuwa na utamaduni huu” alisema Meya Mwita.
Alieleza kwamba “ Jumuiya za kimataifa zimekuwa zikiwatazama waislam wote  kama watu ambao si  salama nakushauri kwamba haki za kibinadamu zizingatiwe kwao kwakuwa wote tunaombwa na Mungu mmoja” alisema Meya Mwita.
Aliongeza kwamba “ wapo watu ambao wanaitumia dini ya kiisilamu  vibaya, nakuchafua watu wengine , lakini tunatakiwa kutambua kwamba kila wote hapa tumeumbwa na mungu mmoja, sasa dini zetu zisitufanye tukashindwa kushirikiana na kuzungumza lugha moja” alisistiza.
Hata hivyo katika hatua nyingine Meya alisisitiza majiji makubwa ya nchi za kiafrika yajielekeze katika kutatua changamoto za watu wake.
Aidha Meya ametumia nafasi hiyo   kuwakaribisha Wailan kuja kuwekeza katika Nchi ya Tanzania sambamba katika kuendeleza fursa za kibiashara.
Hata hivyo mkutano huo umemalizika na kwamba Meya kesho ataelekea jijini Tairan kwa mualiko wa Meya wa jiji hilo ambapo pamoja na mambo mengine huko atatembelea ofisi za umma na kukutana na wadau mbali mbali kwa ajili ya kujadili namna ya kuendesha majiji sambamba na kutatua changamoto.

No comments: