Serikali imewahakikisha
watetezi wa haki za binadamu nchini kuwa
serikali inatambua mchango walionao katika kuhakakisha haki za binadamu zinalindwa na kudumishwa nchini na kuwaahidi
kuwa Serikali itaendelea kushirikiana
nao na kuwawekea mazingira stahiki ya
watetezi wa haki za binadamu kuendelea
kufanya kazi zao kwa utimilivu.
Kauli hiyo ya Serikali
imetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi mjini Dar es salaam katika maadhimisho ya Nne
ya watetezi wa haki za binadamu nchini kwa niaba ya Makamu wa Rais mhe. Samia
Suluhu Hassan.
Katika maadhimisho hayo Prof
Kabudi alizindua taarifa ya hali ya haki za binadamu kwa mwaka 2016 ambayo iliandaliwa na Mtandao
wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania.
Maaadhimisho hayo yameandaliwa
na mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini na kuhudhuriwa na watetezi
wa haki za binadmu kutoka mikoa yote ya
Tanzania Bara na Zanzibar. Pia
yamehudhuriwa na wawakilishi wa malozi
na mashirika ya kimataifa, Wizara na taasisi za serikali
Maadhimisho hayo ya mwaka huu
yalikuwa na kauli mbiu isemayo kuboresha ushirikiano na serikali
No comments:
Post a Comment