Thursday, April 27, 2017

CHETI CHA KUZALIWA KINAWEZESHA MTANZANIA KUPATA HAKI ZA MSINGI-PROF KABUDI


Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba  Kabudi amesemacheti cha kuzaliwa kunamuwezesha mtoto/mtanzania kupata haki za msingi kama raia.
Prof  Kabudi amesema hayo mjini  Dodoma wakati akifungua semina ya wadau kujadili mapitio ya sheria zinazohusiana na usajili wa matukio muhimu ya binadamu nchini.

Amesema ni muhimu kuimarisha harakati za kukuza mwamko wa usajili wa watoto na watanzania kwa ujumla wanapaswa kusajiliwa na kupata vyeti kwani kuwa na vyeti hivyo kutawawezesha kupoata haki zao za msingi .

Amezitaja haki hizo kuwa ni pamoja na kuwa na jina,kupata kazi, kutambulika kama raia, na kuzuia watoto chini ya miaka 18 kuingizwa katika vita, ajira za utroto na hata kushtakiwa kwa makosa ya jinai na kuwekwa rumande na watu wazima.
Prof Kabudi alichukua nafasi hiyo kuihakikisha timu hiyo kwamba atahakikisha sheria hiyo ya usajili wa vizazi, vifo na talaka inafanyiwa marekebisho haraka ili ziweze kwenda na wakati uliopo sasa na hivyo kukuza usajili wa watanzania .

‘Nitahakikisha sheria hii inafanyiowa marekebisho haraka, kwani kuirekebisha sheria hii kutaifanya iendane na wakati na kufanya usajili wa watanzania kuongezeka, hatuna budi kuongeza bidii katika kazi hii ili watanzania wote waweze kusajiliwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa,” alisema Prof. Kabudi.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Kabudi Mweyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini Jaji Aloysis Mujuluzi tume yake iliendeesha utafiti juu ya sheria hiyo ya usajili katika mikoa 13 nchini na kuunganisha na tafiti za sheria mbalimbali ili kuhakikisha maboresho ya sheria hiyo yanazingatia maoni ya wadau mbalimbali nchini.

Alisema wanaifanya kazi hiyo kwa moyo mmoja na watakapoikamilisha tu watamkabidhi Waziri Kabudi ili nae atoe maoni yake kama mdau ili kuweza kuwa na sheria mpya itakayokidhi mahitaji ya wakati uliopo na wakati ujao.
Alisema katika tafiti yao wamegundua kuwa mfumo wa usajili wa raia nchini haujakaa vizuri kwani  mifumo hiyo haiuzungumzi lugha moja na hivyo kuwachanganya watanzania. Aliitaja mifumo hiyo kuwa ni Vitambulisho vya Taifa, kadi ya mpiga kura , hati ya u
Kusafiria na cheti cha kuzaliwa
Alisema umefika wakati sasa kwa mifumo hiyo kuzungumza lugha moja na kuongeza kuwa mifumo yote hiyo ilitakiwa itegemee chetio cha kuzaliwa cha mtu na ndipo waendelee na utaratibu wake.

Alisema kutokana na hali hiyo ndio maana watanzania wachache wapatao asilimia 13.4 tu ndio wenye vyeti vya kuzaliwa   

No comments: