Tuesday, May 30, 2017

DKT.KIGWANGALLA AKABIDHI GARI LA WAGONJWA MKURANGA

Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla mapema jana Mei 28.2017 amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) na vifaa vya Hospitali ikiwmo vitanda na Magodoro katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani. 

Dkt. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, mbali na kukabidhi gari hilo la wagonjwa na vifaa hivyo vya Hospitali kwa uongozi wa Hospitali na Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo hilo, aliweza kufanya ukaguzi wa ghafla kujionea mazingira ya Hospitali hiyo na kubaini mapungufu mbalimbali ambayoo ametoa maagizo kupatiwa ufumbuzi kabla ya kuchukuliwa hatua kwa uongozi wa Hospitali hiyo. 

Miongoni mwa changamoto hizo alizobaini katika Hospitali hiyo ni pamoja na kuwa na mfumo mbovu wa uhifadhi wa taka, pamoja na uchafu katika wodi ya wazazi jambo ambalo linaweza kusababisha hatari ya maambukizi kwa Wagonjwa na wahudumu wenyewe wa Afya. Awali wakati wa kukabidhi gari hilo ambalo limenunuliwa kwa nguvu ya Madiwani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na Mbunge wa jimbo hilo la Mkuranga, Abdallah Ulega aliwataka kulitumia kwa uangalifu wa hali juu huku likitakiwa kufanya shughuli zilizokusudiwa katika kusaidia wananchi wake.

“Nimesikia kileo chenu ambacho ni kupatiwa mashine ya X-Ray na na vifaa vingine muhimu. Wizara yetu inalishughulikia hilo na tunawaomba muwe na imani na Mbunge wenu ambaye amekuwa akinisisitiza juu ya jambo hilo. 

 Hospitali ya Mkuranga ni moja wapo ambayo itafaidika na msaada wa vifaa ikiwemo mashine hiyo ya X-Ray” alisema Dkt. Kigwangalla wakati akizungumza na wananchi mbalimbali ambao pia walipata fursa ya kuuliza maswali katika tukio hilo. Tazama hapa kuona tukio hilo:
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga wakati alipofika hapo kuelekea katika tuko la sherehe ya kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amsikiliza Mbunge wa Mkuranga Mh. Abdallah Ulega katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga wakati alipofika hapo kuelekea katika tuko la sherehe ya kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoka katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga wakati alipofika hapo kuelekea katika tuko la sherehe ya kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Baadhi ya wazee wa Mkuranga
Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga akisoma taarifa
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza katika tuko la sherehe ya kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza katika tuko la sherehe ya kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Baadhi ya wananchi walipata fursa ya kuuliza mswali na kutoa kero zao
Baadhi ya wananchi walipata fursa ya kuuliza mswali na kutoa kero zao
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhi vifaa vya hospitali katika tuko la sherehe hizo za kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikata utepe wakati wa kukaabidhi gari la wagonjwa hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa ndani ya gari la wagonjwa hospitali ya Wilaya ya Mkuranga mara baada ya kulikabidhi
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua masuala ndani ya wodi ya wanawakehospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua masuala ndani ya wodi ya wanawake hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo kwa viongizi wa Wilaya baada ya kukuta hali ya uchafu katika maeneo hayo ya wodi ya wanawake hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akito maelezo namna ya chumba cha upasuaji kinatakiwa kirekebishwe kufuata taratibu zake hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo namna ya mlango wa kuingilia chumba cha upasuaji kutokukidhi viwango hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa katika viunga vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Gari hilo la wagonjwa lililokabidhiwa
Baadhi ya vifaa hivyo vilivuokabidhiwa
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo na Mkurugezi wa Wilaya ya Mkuranga
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akifanya hitimisho wakati akizungumza na waandishi wa Habarimara baada ya kumalizika kwa shughuli ya kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali hiyo ya Wilaya ya Mkuranga, mapema jana Mei 28.2017.

No comments: