Thursday, May 18, 2017

HALOTEL YAPETA KWENYE KESI ILIYOKUWA IKIKABILIWA NAYO

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel imetoa ufafanuzi kuhusu  tuhuma zilizokuwa  zikihihusha kampuni hiyo ya kuisababishia serikali  hasara  ya  shilingi milioni 459 ambapo wao wamehusishwa na vipengele  viwili vya mashtaka.

Mashtaka hayo  ya Halotel ni  kushindwa kutoa taarifa ya  usajili wa kampuni ya mitambo ya UNEX Limited ambayo haikuwa kampuni iliyosajiliwa kikamilifu na TCRA  kwaajili ya kusajili line za simu 1000 zilizouzwa  kwa kampuni hiyo  pamoja na kushindwa kutimiza majukumu yao vizuri ya  kuuza  line za simu 1000.  
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya mtandao wa simu wa halotel Tanzania Bw. Le Van Dai akitoa ufafanuzi juu ya kesi iliyokuwa ikawakabili kama shirika.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Halotel Tanzania  Bw. Le Van Dai  amefafanua juu ya kutokuhusika na  makosa ambayo yaliwahusisha watuhumiwa wengine ambao  ni wateja wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na usimikwaji wa mitambo hiyo.

Alisema kuwa  kampuni hiyo  imekuwa ikiendesha  ikiendesha shughuli zake nchini  kwa kufata sheria na  taratibu zote   za mawasiliano ambazo zinatambuliwa na mamlaka  ya mawasiliano nchini (TCRA).

Bw lai aliongeza kuwa kwa mujibu wa mashtaka  yaliyosainiwa na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali kuwa  Mei 16 mwaka huu ambayo yanayoitaja kampuni hiyo kuhusika na makosa hayo.
Mwanasheria wa kampuni ya Halotel Bw Christopher Masai akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam.

Mwanasheria wa kampuni ya Halotel TZ Bi Fatma Seif akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam
Alisema mujibu kifungu namba 6 na 7 ambavyo havihusishi kampuni hiyo na makosa ya washtakiwa wengine ambao sio wafanyakazi wa kampuni hiyo na  kuongeza kuwa  hawana ushirikiano wowote na kampuni hiyo pamoja na raia hao wa Pakistani zaidi ya kuiuzia laini za simu kampuni hiyo baada ya kuwasilisha nyaraka zisizo halali.

“Sisi  kama kampuni tunafanya kazi kwa usajili na vibali halali vya mamlaka husika  nchini na tumekuwa wawazi na kufata vibali kutoka mamlaka husika pamoja na kufata taratibu zote za kisheria " alisisitiza Dai
Waandishi wa habari wakiwa makini kufuatilia ufafanuzi unaotolewa na viongozi wa kampuni ya halotel TZ mapema leo jijini Dar es salaam     

Waandishi wakiwa kazini.

No comments: