Friday, May 19, 2017

STAR TV YAZUA BALAA- JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LATOA TAMKO ZITO KUSALITI TASNIA YA HABARI,MTANGAZAJI WAO NAYE APONDA


Mahojiano Maalumu yaliyoandaliwa na Star Tv waliyopanga kufanya na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, yamekiponza chombo hicho.

Jukwaa la wahariri Tanzania TEF limekitafsiri kitendo hicho kuwa ni usaliti.
Awali waraka huu ulisambaa kwa kasi ya ajabu mtandaoni

WARAKA YA WAZI KWA UONGOZI WA SAHARA MEDIA GROUP KUHUSU KIPINDI CHA TUONGEE ASUBUHI KINACHOTARAJIA KURUSHWA JUMATATU YA TAREHE 22/5/2017

Anaandika William Bundala

(Kijukuu Cha Bibi K)

Habari ya wakati huu uongozi wa Kampuni ya Sahara Media hususan wahariri  wa Star Tv Mwanza na Dar es salaam,Mimi ni mzima wa Afya tele licha ya hali ngumu ya maisha tuliyonayo kwa kipindi hiki cha mpito.


Mimi naitwa William Bundala jina maarufu Kijukuu Cha bibi K,Ni mtangazaji wa na Mwaandaaji wa Vipindi Radio Free Africa,Nimeamua kutumia nafasi hii kuwaandikia viongozi wangu wa Sahara hususan ni Star Tv.


Ndugu zangu siku za hivi karibuni nimeona kipererushi mitandaoni kikionyesha kuwa Kituo chetu cha Star Tv kitarusha mahojiano ya Mkuu wa mkoa Fulani katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI,Nianze kwa kuwapongeza upande wa jinsi mlivyotengeneza kipeperushi (Cover) na kukisambaza katika mitandao ya kijamii.


Nimeona jitihada za usambazaji katika Magroup ya Whattupp,Instagram,Facebook,Twitter na maeneo mengine mengi,Hakika Tanzania na nje ya Tanzania asilimia kubwa watu wameona mwaliko huu ambao kwa upande wangu mimi sijaona umuhimu wake hata chembe.


Ndugu zangu Star Tv ukweli usiyofichika ni kwamba siku ya kurusha kipindi hiki tutatazamwa sanaa na idadi kubwa ya watu ila idadi hiyo ya watu itakayotutazama ndiyo itakuwa mabalozi wa kuwaondoa wengine wasitazame Tena Star Tv labda watasalia wachache ambao naamini kusalia kwao ni kutokana na Kipindi cha FUTUHI tu.


Ninachoandika hapa naomba kwanza ieleweke ni utashi wangu binafsi na hakuna mtu aliyenisukuma katika hili,na andiko hili lisihusishwe na maswala yoyote ya kisiasa,kidini wala kikabila bali ni katika kujengana na kufanikiwa kuinua kituo chetu.


Ieleweke kuwa kwa sasa tunatakiwa kufanya vitu vingi vya kijamii ili kuwarudisha watazamaji wetu kuwa na imani na chombo chetu,Nasema hivi nikikumbuka namna tulivyokuwa tunasemwa vibaya wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015.


Tumesemwa sanaaa kwenye mitandao ya kijamii lakini zaidi hata sisi tunaopenda kukaa kwenye Stuli ndefu tulikuwa hatuna furaha kutokana na kusemwa sanaa kuhusu kampeni za uchaguzi huo.


Tungali bado tunamalizia kuuguza makovu ya kusemwa vibaya tangu uchaguzi wa  mwaka 2015 naona kila dalili za kidonda cha kusemwa vibaya kurudi tena mara ya pili hii ni baada ya kwenda hewani kwa kipindi hiki ambacho nimeona katika kipeperushi kipya kuwa kitakuwa ni jumatatu.


Ninazo hoja chache za mimi kupinga kipindi hiki kwenda hewani,Siwezi kuzuia kisiende kutokana na nafasi yangu bali naweza kushauri na mkaangalia upya mfanye nini jumatatu kuliko kuruhusu kipindi hicho kwenda hewani.


Ngudu yangu Kaka yangu mshauri wangu wa maswala ya Media Paul Mabuga najua sanaa uwezo wako katika Tasnia ya habari je hili swala mmelichuja na kuona faida na hasara zake kwa Chombo chetu cha Star Tv?


Kaka yangu rafiki yangu Moses Buhilya Program Manager Star Tv kama sijakosea cheo,Je umekaa chini na waandaaji wa hayo mahojiano kujua nini wanahitaji kumuhoji mkuu huyo wa mkoa?


Sitaki kuongea chochote kwa wapiga picha ambao watashika camera siku hiyo kwani katika hili sijaona kama wana madhara katika kutekeleza majukumu yao.


Ninayo mambo machache ya kuhoji na kushauri kuhusu kipindi hiki:-


(1)Naomba kurudia tena kuwa tutafanikiwa sanaaa kutazamwa na watanzania wengi na hata wasiyo watanzania kutokana na mambo lukuki ambayo watanzania wanataka kuyajua kutoka kwa mgeni atayehojiwa siku hiyo,Lakini katika hili naomba kuwaambia kuwa baada ya kipindi kuisha watazamaji hao watakimbia,Ni vigumu kujua watakimbiaje maana hatuwezi kujua kama watatazama au laa.

(2)Mtu anayehojiwa namfahamu vizuri katika zana nzima ya kuongea anaweza sanaa kuongea na anaijua Media vilivyo,Hofu yangu inakuja hao watu ambao mmewateuwa kufanya naye mahojiano,Hofu hii inakuja kutokana na ukweli kuwa Mgeni atabadilika kuwa mwendesha kipindi na waandesha kipindi kugeuka kujibu maswali na kuitingisha kichwa kukubali atakachokisema mgeni kutokana na uwezo wake alionao.Sibezi kama watakaohoji hawajui HAPANA bali kama mtafanya akikisheni IQ ya watangazaji iwe kubwa sanaa katika kuhoji na kuuliza maswali kuliko IQ ya Mgeni.


(3)Jambo la tatu ambalo ndiyo kubwa katika waraka huu ni kutaka kujua kama Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) tayari wameruhusu Huyu mgeni anayetaka kohojiwa jumatatu ahojiwe,maana nakumbuka walitoa tamko hakuna chombo kinachoruhusiwa kutoa habari zake,Niwakumbushe tu kuwa agizo hilo la baraza la wahariri Tanzania (TEF) kwa kushirikiana na Klabu ya waandishi wa habari Dar es saalam (DCPC) lililoungwa mkono na umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) lilitolewa Tarehe 22/3/2017.


Katika Agizo hilo walibainisha mambo ambayo waliyohuzinishwa nayo yaliyofanywa na Mgeni huyo mnayetaka kumwalika na kisha kutoa hatua tatu za kuchukua

Katika barua hiyo walisema,Tafadhali Soma hapa chini kupitia link ya Mpekuzi

http://www.mpekuzihuru.com/2017/03/tef-yamtangaza-makonda-adui-wa-uhuru-wa.html

Bada ya kusoma link hiyo tujiulize kabla jumatatu haijafika je Waliotoa agizo hilo wamesharuhusu kufanya naye vipindi? Na kama bado hawajaruhusu je sisi Star Tv agizo hilo halituhusu na kama linatuhusu je wapi tunapata nguvu ya kwenda kinyume na Agizo la baraza la wahariri Tanzania?

(4)Tangu niajiriwe hapa Sahara Media tangu Mwezi wa 10 mwaka 2013 sikuwahi kuona mahojiano ya mgeni huyu anayetarijiwa kufanya nasi kipindi maalumu cha Toungee Asubuhi siku ya jumatatu,Nimezoe kuona taarifa za habari tu ambazo zinaandikwa na waandishi wetu wa Dar es salaam lakini vipindi vya namna hii nimeona katika Tv zingine za Dar es salaam na siyo hapa kwetu,Je nini kimetokea mpaka mahojiano haya yafanyike hapa kwetu?..Nakumbuka sisi Radio free Tuliwahi kumpigia simu tukihitaji kufanya naye mahojiano kuhusu kauli yake ya kutaka Benki impe maelezo kuhusu inawezekanaje watunishi hewa kuchukua mishahra kupitia Bank? lakini hakutupa ushirikiano badala yake alitujibu vibaya kwa kutwambia sisi hatujui mkuu wa mkoa ana mamlaka gani na kuongeza kuwa ndiyo mana Hatuendelei.Je leo ametuona Sahara Media na Vyombo vyake tunajua mamlaka ya mkuu wa mkoa na ndiyo mana ametaka kufanya mahojano na sisi?


(5)Kuna swala linaandikwa mitandaoni na baadhi ya watu kuwa waandaaji wa kipindi hiki cha jumatatu wanatafuta Kujijenga wenyewe na siyo kukijenga kituo,Mimi sitaki kuamini hili ila lisemwalo na mtu mzima usilipuuze,Nashindwa kukataa kwa asilimia 100 kutokana na promotion ya hii kitu nashawishika kukubali,Kwanza nina imani Mgeni atakuwa katika ofisi ya Dar es salaam na wengine watakuwa ofisi za Mwanza,Swali linalokuja kichwani mwangu kwanini kwenye kipeperushi wawekwe watangazaji wa wa Mwanza ambao hawatakuwepo na Mgeni studio? Je picha za watu watakaokuwa studio ya Dar es salaam hazipo au hawana umuhimu katika kipererushi hicho? Kwanini tusiamini kuwa hiki kipindi kinatafuta umaarufu kumjenga mtu na siyo kituo?


(6)Amini nawaambia mara baada ya kipindi hiki kurushwa vyombo vyetu vitashambuliwa sanaaa na kutengwa,Mkuu wangu boss wangu Osolo Nyawanga wewe ni Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza(MPC) Ambao mpo chini ya Umoja wa klabu za waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Ambao nao wameunga mkono kuwa hakuna chombo kinachoruhusiwa kutoa habari za mtu huyu,Je Kiongozi wangu Osolo umelitazama hili kwa jicho la FAIDA na HASARA?


(7)Nduu zangu viongozi baada ya kipindi hiki kuruka tujiandae kuandikwa kwenye mitandao  ya kijamii na kusemwa kwa kwenda kinyume na vyombo vingine ikiwa ni pamoja na kuanza kuvuliwa nguo viongozi,watangazaji na kampuni kwa ujumla,Usije kushangaa yakiandikwa mengi mpaka kuhusu Kiwango cha elimu cha watu waliondaa mahojiano hayo,Machache yameanza kusemwa kuwa mmoja kati ya watu watakaongoza kipindi hicho sijui wa Dar au Mwanza hana cheti badala ya kushindwa kumaliza masomo ya Certificate katika moja ya chuo cha habari kanda ya ziwa,Kama yameeanza haya kipindi hakijaruka mnategemea nini kipindi kikiruka? Chonde chonde Viongozi wa Star Tv……”YA NGOSWE TUMWACHIE NGOSWE”.


(8)Swala lingine tusiangalie watazamaji wa siku moja ila angalieni je Tv inatakiwa kuishi miaka mingapi?,Tumesahau kuwa mwaka 2015 wakati wa Uchaguzi gari letu  la Mahidra lililokuwa likiendeshwa na dereva Gerlad Swai lilipigwa Mawe eneo la Pasiansi na tukaamua kubandua Lebel (Vipeperushi ) kwenye magari vinavyoonyesha magari ni ya Kampuni ya SAHARA MEDIA,Je hili mmelisahau wenzetu?Tafadhali tupime faida tutakayopata kama chombo Star Tv na hasara yake kwetu kama kampuni kabla ya kuangalia kitu kimoja tu kuwa tutatazamwa sanaa.


(9)Mimi sina piamizi na wazo la kurusha kipindi hiki,ila hofu yangu ni hayo ambayo nimeyaeleza hapo juu,kama kampuni na uongozi wa Star Tv mtakuwa tayari kupambana na hayo ambayo naamini siyo yote  yatatokea niwatakie kila la kheri na mimi nitakuwa mtu wa kwanza kuangalia kipindi hicho.Na kama kuna maagizo maalumu kutoka ngazi ya juu ya Serikali naomba waraka huu upuuzwe kwa nguvu zote lakini kama hakuna maagizo ni maamuzi tu ya waandaaji wa kipindi cha TUONGE ASUBUHI Nawasihi angalieni upya swala hili kabla ya jumatatu kufika.


(10)Mwisho lakini si kwa umuhimu,Naomba nisijadiliwe vibaya na kuonekana nipo kinyume na kampuni iliyoniajiri,Bali mawazo haya yapokelewe na yafanyiwe kazi kama yanafaa,Sina chuki na Mgeni,Sina chuki na watangazaji watakaohusika kuendesha mahojiano wala sina chuki na kampuni yangu,Bali kwa akili zangu nimewaza nikaona hili swala litatugawa na kuibua mwanzo mpya wa mengi ndani ya kampuni yetu.


MY POINT:

“DON’T PUT YOUR MOUTH ON MOTION, WHILE YOUR BRAIN IS ON GEAR”

Ndimi

William Bundala

(Kijukuu Cha Bibi k)

0767-942570

0786-942570

E-mail bundala.william@yahoo,com


www.kijukuu.com

No comments: