Paul Mikongoti akiwasilisha Report ya haki za binadamu ya mwaka 2016 iliyozinduliwa jana na kituo cha sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania LHRC |
Kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania kimezindua Ripoti yake ya Haki za Binadamu kwa mwaka 1016. Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es salaam na mgeni rasmi alikuwa ni Jaji Msataafu wa Mahakama ya rufaa Eusabia Munuo.
Akichanganua Ripoti hiyo Mwanasheria kutoka LHRC Bw. Paul Mikongoti alisema kuwa
ripoti hiyo imefanyika kupitia njia mbalimbali za uchunguzi mpaka kuweza
kukamilika.
Njia ya kwanza ilikuwa ni kutembelea maeneo husika na kuongea na
wahusika lakini pia njia nyingine ni kuchukua tafiti zinazofanywa na mashirika
mbalimbali kama TWAWEZA ,TGNP ili kuweza kupata data zilizoweza kusaidia
uandishi wa ripoti hiyo. Na pia ripoti hiyo ililenga sehemu mbalimbali ikiwa Nyanja
za kisiasa kijamii na watu wenye mahitaji maalum.
Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo Jaji Msataafu Eusebia Munuo akizungumza na wageni waalikwa katika Hafla ya uzinduzi wa Riport ya Haki za binadamu |
Alisema kuwa Tangu kuingia kwa awamu ya tano madarakani
kumekuwepo kwa ukiukwaji wa haki za kisiasa na ni kutokana na Raisi Magufuli
alipokataza mikutano ya kisiasa na baadae hata kufikia kukataza vikao vya ndani hali iliyoonekana kuchochea baadhi ya mambo kama (UKUTA) ulioundwa na chama
cha CHADEMA kupinga udikteta nchini na kuweza kuona polisi wakifanya mazoezi na
magari ya kuwasaha hali ambayo iliwanyima wanasiasa haki yao ya kikatiba.
Kwa upande wa haki za kiraia, Mikongoti amesema bado kuna
ongezeko la matukio ya watu wanaojichukulia sheria mkononi kuua raia ambapo
matukio 705 yaliripotiwa, ukiukwaji wa uhuru wa kujieleza ukilinganisha na
ilivyokuwa mwaka 2015 baada ya kuanza kutumika kwa sheria ya makosa ya mtandao
ya mwaka 2015 na ya huduma ya vyombo vya habari 2016.
Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo Jaji Msataafu Eusebia Munuo akizindua Riport hiyo |
Hata hivyo, ripoti hiyo inaonyesha kupungua kwa vifo
vitokanavyo na ajali, mauaji ya albino, na yanayotokana na imani za kishirikina
hasa vikongwe hali inaonyesha kuwa mkoa wa shinyanga matendo hayo yamepungua na
kwa sasa mkoa unaoongoza ni tabora ukufuatiwa na mbeya.
Na kwa watu wenye mahitaji maalumu matendo ya kubakwa na
kulawitiwa yakiwa yameshamiri kwa kiasi kikubwa na mkoa unaaongoza ni Dar es
salaam, Mbeya, Morogoro Pia katika mikoa ya Arusha.Matukio
mengine ya kupigwa na kunyimwa haki zao za msingi bado mikoa ya kanda ya ziwa
bado inaongoza.
Meza kuu Ikionyesh Riport hiyo baada ya kuzinduliwa. |
Aliongezea kusema kuwa katika nafasi ya uongozi kwa wanawake
wamebanwa kwa kiasi kikubwa kwa mfano awamu iliyopita kulikuwa na wanawake wengi
wakuu wa mikoa. lakini kwasasa wamepunguzwa sana pia hata katika mawaziri na
manaibu waziri wapo wachache sana.
Katika upatikanaji wa huduma bora za kijamii mikongoti
alisema kutokana na swala la elimu bure hali hii imesababisha kukosa waalimu.
na kwa upande wa afya wauguzi na vitendea kazi vimekosekana kwenye hospitali
hususani vijijini.
Wageni mbalimbali wakifwatilia kwa ukaribu. |
No comments:
Post a Comment