Wednesday, May 3, 2017

CHADEMA Yatangaza Majina 6 ya Watu Watakaogombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imewateua washiriki sita kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala).

Katika kikao kilichofanyika jana mjini Zanzibar walioteuliwa ni Profesa Abdalla Safari, Salum Mwalimu, Ezekiel Wenje, Josephine Lemoyan, Lawrence Masha na Pamela Massay.

Taarifa ya leo iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene imesema wateule hao watakamilisha hatua zingine za uteuzi kwa mujibu wa utaratibu, Kanuni za Bunge na Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki.

Masha na Wenje, walishiriki uchaguzi uliofanyika Aprili 4 ambao Chadema ilipeleka majina yao pekee jambo lililozua mjadala bungeni na kuhitimishwa kwa wao kupigiwa kura za Hapana.

Katika uchaguzi huo, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waliwachagua wajumbe saba wa Eala.

Kwa upande wa CCM, walioshinda ni Fancy Nkuhi, Happiness Legiko, Maryam Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngwaru Maghembe na Adam Kimbisa na kutoka CUF iliyokuwa na wagombea watatu kwa ajili ya nafasi moja, aliyeshinda ni Mohamed Habib Mnyaa akiwashinda Twaha Taslima na Sonia Magogo.

No comments: