Monday, May 22, 2017

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU KIMETOA TAMKO JUU YA MAUJI YANAYOENDELEA KOTE NCHINI

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu  (LHRC) kimekemea vikali vitendo vya mauaji vinavyoendelea sehemu mbalimbali kote nchini .

Akiongea na waandishi wa habari  Kaimu Mkurugenzi mkuu Bi. Anna Henga  alisema kuwa vitendo vinavyoendelea kwa sasa vya mauaji ya polisi pamoja na Raia ni ukiukwaji wa haki za binadamu na vinatakiwa kukemewa haraka iwezekanavyo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu Bi. Anna Henga akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam

Tumeweza kuona matukio yaliyotokea sehemu mbalimbali ikiwa Tanga, Geita pamoja na yanayoendelea huko kibiti mkoani pwani yanayohusisha mauaji ya viongozi wa vijiji ikiwa kijiji cha nyabuda,  mkandawala, kaza moyo na mwenyekiti wa ccm makondeko pamoja na mkuu wa kituo cha polisi.
Hali hii inawafanya wananchi wa maeneo hayo kuweza kuishi kwa woga kutokana na vitisho vya askari wenye bunduki wakipita pita maeneo yao ya kazi. Hali hii inadhorotesha uchumi wanchi kutokana na raia kushindwa kufanya shughuli zao kwa uhuru kuhofia kukamatwa na waliowengi kushindwa kwenda hata mashambani na wengine kazi zao zinaanza kuchanganya kuanzia usiku kama chipsi lakini wanashangazwa na serikali kutoa onyo kuwa kwa maeneo hayo kwepo mwisho saa 12 jioni.

Mkurugenzi wa ufuatiliaji ukiukwaji wa haki za binadamu na uwajibikaji (DHA) Felista Mauya akitilia mkazo alichokiongea kaimu mkurugenzi mtendaji

Kituo cha sharia na haki za binadamu kimetoa mapendekezo ikiwemo kurudishwa kwa polosi jamii kwa kuweza kubaini watendaji wa haya ni nani?.

Askari kuweza kuboreshewa mafunzo yanayoendana na wakati uliopo wa sayansi na teknolojia na sio kutumia nguvu kwani wanowaumiza ni raia na siyo waalifu kama wanavyodhani.

Kupelekwa watafiti waweze kuchunguza kuwa wanofanya mambo haya wanatoka wapi na sio kukurupuka na kuanza kuonea raia kana kwamba wao ndio wanotekeleza mauaji hayo.

Na wananchi hususani vijana kupewa elimu ya uraia ili waweze kuwa na uzaredo na nchi yao  na kuacha kujichukulia sharia mikononi.


baadhi ya waandishi walioudhuria press hiyo


No comments: