Friday, May 26, 2017

Kwa wnafunzi wote--TCU YATANGAZA MFUMO MPYA WA KUDAHILI WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Vyuo Vikuu nchini kwa mwaka wa masomo 2017/2018 watatumia mfumo mpya wa udahili tofauti na ule uliozoeleka wa kuchaguliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Haya yamebainishwa katika taarifa ya TCU iliyotolewa juzi  ambapo  imesema kuwa wanafunzi wote wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu kwa mwaka  wa masomo 2017/2018 watatumia mfumo mpya ambao unawataka kwenda vyuoni moja kwa moja kuomba nafasi.

Hivyo,taarifa hiyo imewataka wanafunzi  waliomaliza kidato cha sita kwa mwaka wa masomo 2017/2018 kuomba nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu moja kwa moja vyuoni kuanzia tarahe 22 Julai 2017 hadi 13 Agosti 2017.

Sifa za kujiunga kwa wanafunzi wote ni kama ifuatavyo…
==> Isome taarifa ya TCU hapo chini


No comments: