Friday, May 26, 2017

TANZANIA UGANDA ZASAINI MKATABA UJENZI BOMBA LA MAFUTA

 Serikali za Tanzania na Uganda zimetoa saini makubaliano yatakayowezesha ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini.
Ujenzi huo unatarajiwa kuwa umekamilika wa ifikapo mwaka 2020.  
Mkataba wa mradi wa Bomba la Mafuta kati ya Serikali ya Tanzania na Uganda (Intergovernmental Agreement- IGA) umesainiwa leo tarehe 26 Mei 2017 Jijini Kampala, Uganda na kuhudhuriwa na Mawaziri,  wanasheria wakuu wa nchi hizo,  makatibu wakuu na maafisa wengine wa serikali hizo mbili. 
Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.  Prof. Palamagamba Kabudi  na Waziri wa Nishati na maendeleo ya madini wa Uganda Mhe. Eng Irene Muloni
Mkataba huo umesainiwa kufuatia Tamko la pamoja lililosainiwa kati ya marais wa Tanzania na Uganda  Mei 21 mwaka huu jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo Profesa Kabudi amesema kusainiwa kwa mkataba huo kunadhihirisha dhamira ya dhati waliyonayo viongozi wakuu wa nchi hizi ambao wamepania kuboresha maisha ya wananchi katika ukanda huo utakapopita bomba hilo.
Pia amewapongeza wataalamu wa pande zote walishiriki kufanikisha mkataba huo hadi kusainiwa ikiwa ni pamoja na makatibu wakuu wa nchi hizo ambao waliwasimamia vyema wataalamu hao. 
Amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutatokea manufaa makubwa kwa wananchi wa nchi hizo hasa katia maeneo nayo bomba hilo litapita
Amewataka baadhi ya manufaa kuwa ni pamoja na kutoa ajira kuanzia wakati wa ujenzi wa bomba kwa watu kati ya 6000 hadi 10000. Kupatikana kwa urahisi kwa mafuta kwa ajili ya nchi hizo,  za Afrika Mashariki na Kati na hata Afrikakwa jumla.


No comments: