HABARI ZA KIJAMII

MEYA DAR, ISAYA MWITA AONGOZA MASHEKHE KATIKA DUA YA KUKARIBISHA MFUNGO WA RAMADHANI


Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita, jana alioongoza mashekhe ikiwa ni utamaduni wa kukaribisha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Dua hiyo iliyofanyika Tambaza makaburini, Upanga Mashariki Jioni , iliaambatana na dua za kuwaombea marehemu wote ambao walikuwa vipenzi vya mtume na watumishi wa Quruan hususani aliyekuwa mtabiri wa Nyota hapa nchini, Shekhe Yahya Hussein aliyetangulia mbele ya haki.

  kipenzi cha Mtume Muhamad (S.a.W), ambaye pia ni mjukuu wa marehemu Shekhe Yahya Hussein, Yahya Hussein wakati akisoma Quruan Tukufu  katika Makaburi ya Tambaza Jijini Dar es salaam jana 
Katika Dua hiyo, tulishuhudia baadhi ya vipenzi vya mtume, wakisoma Quruan Tukufu  pamoja na mashairi mbali mbali, miongoni mwa vipenzi vya mtume ambao walisoma Quruan ni pamoja na Hassan Nassoro Amrani, Hussein Nassoro, Mohamed Nassoro Amrani, halikadharika na Yahya Hussein ambaye ni mjukuu wa marehemu Shekhe Yahya Hussein.
Aidha akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Shekhe Yahya Hussein Foundation,Mohamed Nassoro Amrani, alisema kuwa , lengo la dua lilikuwa ni kuwaombea marehemu wote waliojitoa kwa maslahi ya dini ya kislamu pamoja na watumishi wa Quruan Tukufu akiwemo Shekhe Yahya Hussein.
Pia aliongeza kwa kusema kuwa, pamoja na dua hiyo lengo walilenga kuwa na dua ya pamoja kwa ajili ya kuukaribisha mfungo wa mwezi mtufu wa ramadhani unaotarajia kuanza hivi karibuni ambapo waisalamu wote watatkiwa kufunga mwezi huu ili kuweza kukamilisha nguzo ya kislamu katika nguzo tano walizo nazo.

.Meya Isaya Mwita, akipokea dua jana wakati wa kisomo cha kuwaombea marehemu na kukaribisha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani katika viwanja vya Tambaza Makaburini  Jijini Dar es salaam jana 
“Tumekuwa ni utaratibu wetu wa sisi waislamu pamoja na Foundation ya kufanya dua kila mwaka kwa ajili ya kumkumbuka mtumishi wa Quruan Tukufu marhemu Shekhe Yahya,mbali na kumkumbuka ni utamaduni wetu kila ikariapo mfungo wa mwezi wa ramadhani tunakuwa na dua maalumu ya kuukaribisha na kukumbusha mazuri ambaayo tunatakiwa kufanya na kuyakataza yale mabaya ambayo yalipingwa katika kipindi hiki ili kuendeleza dhima nzima ya Uislamu na mazingatio yake kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha Quruan”, alisema Amrani  
Pia akisoma risala fupi mbele ya mgeni rasmi, Yusuph Momba, alisema anawapongeza Pepsi kwa mchngo wao wa kutoa mahema pamoja na kujenga ukuta kwani eneo hilo lilikuwa ni eneo la maovu kama vile uvutaji bangi, vibaka na vitendo vingine visivyo na usalama kwa jamii,  lakini mbali na msaada huo bado wana deni kwa mkandarasi hivyo wamemuomba Mstahiki Meya aliangalie swala hili kwa kina na kuweza kuwasaidia kulipa deni hilo.Meya Isaya Mwita, (kati kati),i mototo wa shekhe Yahya Hussein, Hassan Yahya Hussein, pamoja na mdogo wa marehemu Shekhe Yahya, Omary Yahya Hussein , Imamu wa Masjid Farouq Bakwata makao makuu, Mwita Abubakari
Akizungumza na waandishi wa habari, Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita, aliwataka waislamu kuendeleza mema aliyoyaacha mtume Muhamad (sw) huku na kilinda heshima ya watumishi waliotangulia katika kuhakikisha umma wao unakuwa salama na kuimarisha  mshikamano wao katika kuelekea mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani unaotarajia kuanza mwiahoni mwa wiki hii  ili kutimiza nguzo tano za uislamu.
“Changamoto nimezisikia naombeni mnitajie deni lililopo naweza kulilipa lote au kulipunguza pia wale walichonacho pia wajitahidi kutoa kwa ajili ya kujenga umma wao waache ubahili wakiwa bahaili hata matumizi yao mungu hata yanyoosha kwa njia slama watajikuta wakifanya vitu vizuri ambavyo havidumu hivyo nawaaombeni katika kuelekea mwezi huu tuanye mema “,alisema Meya Mwita
Na Yusuph Mwamba

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.