Monday, May 8, 2017

Meya wa Dar azindua ujenzi wa madrasa Mujahirina uliopo mtaa wa Mongolandege kata ya Ukonga

Mstahiki Meya  wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita (kulia) akiwa meza kuu, kushoto ni Diwani wa Kata ya Ukonga, Juma Mwipopo, wakiwa meza kuu tayari kwa kuanza kwa hafla hiyo mara baada ya kutoka katika dua iliyoandaliwa na Shekh Abdul Hamid ikiashiria kuanza salama na kumaliza salama jana.
Inline image 1

Inline image 2
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam, Mh:  Isaya Mwita, akiambatana na viongozi wa dini wakielekea katika uzinduzi wa  ujenzi wa madrasa Mujahirina uliopo mtaa wa Mongolandege kata ya Ukonga Jijini Dar es salaam jana , ambapo ujenzi huo ulifanikishwa kwa kiasi kikubwa na  nguvu ya wazazi  wakishirikiana na viongozi wa dini katika mtaa huo.

Inline image 3
Mstahiki  Mstahiki Meya Isaya Mwita (aliye vaa koti jeusi) , akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo hilo umekamilika,Inline image 4
Mstahiki  Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita, akizungumza na waandishi wa habari jana katika uzinduzi wa Madrasa Mujahirina, uliopo Kata ya Ukonga, mtaa wa Mongo la Ndege huku akafafanua  kuhusiana na mtazamo  walionao Serikali kataika kusaidia maendeleo ya dini hapa nchini ili kujenga uhusiano wa kukuza amani pamoja maadili mema kwa kizazi cha Tanzania na hatimaye kufanikisha malengo yetu na Serikali kwa ujumla,
Inline image 5

Mstahiki  Viongozi wa dini pamoja na waratibu wa maonesho ya Madrasa, na wadau mbalimbali wa maswala ya elimu ya dini, wakiwa pamoja na Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita (wa tatu kutoka kulia) wakiwa ndani ya jengo la Madrasa Muhajirina,  wakati wa dua maalumu  iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Rahma Foundation, Shekh Abdul Hamidi.

Inline image 6
 picha 67 . Meya Isaya (wa tatu kutoka kulia ) pamoja na Viongozi wa dini wakijiandaa kutoka ndani ya chumba cha Madrasa hiyo mara baada ya dua mahususi iliyosomwa na Shekh Abdul Hamidi kwa ajili ya uzinduzi wa Madrasa Mujahirina  kumalizka.
Inline image 7

. Mstahiki Meya Isaya (katikati mwenye koti jeusi) , akisalimiana  na baadhi ya  Viongozi wa dini, waratibu wa maonesho ya Quruan katika Madrasa Mujahirina jana  mara baada ya dua kukamilika


Inline image 8
Mstahiki  Meya Isaya Mwita (kushoto) wakielekea katika meza kuu mara baada ya kukamilika kwa dua

Inline image 9
Mstahiki Meya  wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita (kulia) akiwa meza kuu, kushoto ni Diwani wa Kata ya Ukonga, Juma Mwipopo, wakiwa meza kuu tayari kwa kuanza kwa hafla hiyo mara baada ya kutoka katika dua iliyoandaliwa na Shekh Abdul Hamid ikiashiria kuanza salama na kumaliza salama jana.

Inline image 10
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
Meya  Mwita alitoakauli hiyo mwishoni mwa wiki Meya Mwita alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika uzinduzi Madrasat Muhajiriina ambapo pamoja na mambo mengine alisema kwamba ili kujenga Taifa lenye viongozi wadilifu , wazazi hawana budi kuwajenga kwenye misngi ya elimu ya dini ,elimu dunia.

...............................................
MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amechangia shilingi milioni 1.5 na mifuko 100 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa Madrasat ya Muhajiriina iliyopo Gombo la Mboto katika halmashauri ya Manispaa ya Ilala.  
            
Aidha Meya amewataka wazazi kulea watoto katika misingi ya kidini ili kutengeza Taifa lenye viongozi walio wadilifu, wachamungu na wenye hofu ya mungu.

Meya Mwita alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika uzinduzi Madrasat Muhajiriina ambapo pamoja na mambo mengine alisema kwamba ili kujenga Taifa lenye viongozi wadilifu , wazazi hawana budi kuwajenga watoto kwenye misngi ya elimu ya dini na elimu dunia.

Alifafanua kwamba wazazi hususani wa kina mama ndio ambao wanatakiwa kuwaangalizi zaidi  watoto wao, kutokana na  muda mwingi hukaa nao karibu.

Alisema   kuwa muda huo ambao hukaa na watoto wao, wautumie sio kufundisha mambo ya nyumbani tu, lakini pia hata kwenye  misingi ya kimaadili ya kidini.

“ Mtatengeneza Taifa baya kama wazazi mtashindwa kuwaeleza watoto wenu mambo muhimu yenye maadili yanayofuatana na misingi ya dini, leo hii hapa tunaona watoto mmewavisha mavazi mazuri yenye heshima, lakini mkifika nyumbani mnawavalisha mavazi ambayo hayana heshima, hili ni tatizo” alisema Meya Mwita.

Lazima tusimame kwenye misingi ambayo itawajenga watoto wenu hata huko badae ambapo hamtakuwepo, leo hi mkiwa hai, wenyenguvu msiwajengee misingi mibovu.
“ Leo hii ukimwambia kiongozi acha rushwa, ufisadi hawezi kukusikia kwakua tangu awali hakujengewa wala kulelewa kwenye misingi ya uadilifu” alifafanua Meya Mwita.

Aliongeza kwamba” kila mzazi hapa alipo, kama ulimpeleka mwenyewe matoto wako kujifunza elimu hii ya dini, sasa niwakati pia wakumsimamia ili aweze kuyaishi haya ambayo ameyapata leo” alifafanua.

Katika hatua nyingine Meya Mwita aliwataka vijana waliofikia hatua ya kuoa, watimize wajibu wao na kuacha kusingizia hali ngumu ya kimaisha.

Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana ambao wamefikia umri wa kuoa , kuwanafamilia lakini wanashindwa kufanya hivyo kutokana na kukwepa majukumu na hivyo kusingizia kuwepo kwa hali ngumu ya kimaisha.

“ Tunalowimbi kubwa la vijana ambalo halitaki kujitegemea ,kufanya kazi,  kijana anamiaka kuanzia 25 hadi 35 yupo nyumbani kwa baba na mama , anakwambia hawezi kutoka kuanza maisha mengine kwa sababu hali ya maisha ni ngumu, nahao hao ndio wanajiingiza kwenye makundi ya kihalifu, sasa huko tulipo tunatakiwa kutoka.

“ Hakuna maisha marahisi wala magumu, tunatakiwa kujenga utamaduni huo, msikubali kujibweteka kwa kisingizo cha maisha magumu halafu mnajiingiza kwenye makundi mabaya, jifunzeni kujitegemea” alisisitiza.



Mstahiki  Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita (kushoto) wakijaribu kubadilishana mawazo na Shekh Abdul Hamid (kulia)ambaye ni mshauri wa maswala ya elimu ya dini, mbali na mshari pia ni Mwenyekiti wa Rahma Foundation iliyopo Jijini Dar es salaam makutano ya Morogoro Road na Bibi Titi katika hafla ya uzinduzi wa Madrasa Muhajirina uliofanyika jana Kata ya Ukonga, Mtaa wa Mongolandege.

No comments: