Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh Hemed Jalala akizngumza na wanahabari Nje ya semina hiyo kuhusu malengo yake. |
Na Exaud Mtei
Vijana nchini Tanzania
wametakiwa kutumia dini zao kama viungo vya kudumisha Amani,utulivu,na
upendo uliopo sasa badala ya kutumia
dini zao kutengeneza migogoro na mifarakano katika jamii jambo ambalo lina
madhara makubwa katika ustawi wa taifa kwa Ujumla,
Kauli hiyo imetolewa na
Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la
Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh Hemed Jalala wakati wa semina maalum iliyofanyika
chuo kikuu cha Dar es salaam Ukumbi wa Nkuruma yenye lengo la kujadili kwa
pamoja namna ya kumuunganisha Mwanadamu na dini yake.na mwanadamu kutambua Tunu
zilizopo katika dini yake.
Sheikh
Jalala amesema kuwa Dunia kwa sasa inakabiliwa na vita ya wenyewe
kwa wenyewe ambayo katika nchi nyingi dini imekuwa kichocheo kikubwa cha migogoro
na migongano hiyo jambo ambalo amesema semina hiyo imeamua kuwakutanisha Vijana
Pamoja na wataalam mbalimbali kuwakumbusha namna bora ya kuitumia dini yao
kulinda Amani na kuepuka migogoro kama hiyo.
“Tanzania inasifa ya Amani,
upendo, utulivu, kuheshimiana, kutokubaguana, hivyo vijana tunahitajika
kuhakikisha kuwa tunaenzi Tunu hizi kwa hali na mali ili tuendelee kuwa na sifa
ya kisiwa cha Amani duniani”alisema Kiongozi huyo wa Dhehebu la Shia nchini.
Washiriki wakichangua mada |
Semina hiyo
ilihudhuriwa pia na Wataalam mbalimbali akiwemo Mwanafalsafa wa chuo kikuu cha
Dar es salaam Dr Josephat Muhoza ambaye kwa upande wake amewataka watanzania
kutanguliza Ubinadamu mbele na kisha dini zao baadae kwani kwa kufanya hivyo
watakuwa wamejiepusha na migogoro kama inayoshughudiwa katika mataifa mengo
duniani.
No comments:
Post a Comment