HABARI MPYA

ZITTO ATUMA SALAM ZA RAMBI RAMBI VIFO VYA WANAFUNZI


 TUNAWAPA POLE WALIOFIWA KATIKA AJALI YA WANAFUNZI ARUSHA
KIONGOZI wa chama cha  ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, amesema chama chake  kimepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi zaidi ya 20 pamoja na waalimu wao waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha

Akitoa salama za rambi rambi baada ya kupata taarifa ya vifo hivyo Zitto,alisema Taifa limepoteza nguvu kazi ambayo si rahisi pengo lake kuzibwa

Amewapa pole waalimu wa shule ya awali na Msingi ya Lucky Vicent,wazazi wa watoto ndugu jamaaa na marafiki ambao wamepoteza vipenzi vyao

Amewaombea kwa mwenyezi Mungu majeruhi  majeruhi wapone haraka na waweze kuendelea na masomo yao mpaka wafikie malengo wyaliyotarajiwa.

ACT Wazalendo tumesikitishwa na vifo hivi vya watoto wetu pamoja na walimu wao, tunawapa pole ndugu jamaa na marafiki  Mwenyezi Mungu awape nguvu ya kuhimili kipinfi hiki kigumu kwao

Mwenyezi Mungu aiweke roho za marehemu mahali pema peponi, Amini

Imetolewa na

Abdallah Khamis
Afisa Habari
06/05/2017

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.