HABARI MPYA

BREAKING NEWS-AJALI MBAYA LORI LIMEACHA NJIA NA KUANGUKIA KWENYE RELI NA TRENI LIMEKOSA PA KUPITA


Ajali hiyo imetokea muda huu eneo la Tabata Mwananchi baada ya lori aina ya Scania lenye namba za usajiri T963 DFN kuacha njia na kusababisha Treni ya TRL inayofanya safari zake toka Ubungo kwenda Stesheni kukwama kwa muda usiojulikana.

Gari iliyopata ajari na baadhi ya mashuhuda wakisubiri muafaka
Baadhi ya mashuhuda wanasema kuwa ni uzembe wa Dereva alikuwa kwenye mwendo mkali sana na baadae akaliingia tuta hivyo kufanya gari hilo kuacha njia na kwenda kuharibika mbele ya barabara ya Treni. Treni hiyo iliyotoka ubungo ikielekea Stesheni  imeshindwa baada ya kukosa njia ya  kupitia..

Lakini ajali hiyo haikuweza kuuwa watu bali gari imeharibika kwa sehemu ya mbele na kushindwa kutembea. Na mpaka sasa abiria wote kwenye Treni wameshuka na kuchukua magari ya kuwafanya wawahi safari zao. 

Treni ya TRL ikisubiri gari itolewe iweze kuendelea na safari zake

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.