BURUDANI

QUEEN OF DAR ES SALAAM YA CHEMICAL YA ZUA MZOZO MKUBWA

Msanii wa Bongo Fleva, Chemical amesema wimbo wake wa Queen of Dar es Salaam hajauandika kwa ajili ya watu fulani kama watu wengi wanavyodhani.

Rapper huyo amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One, kuwa yeye amerudia kile ambacho walifanya Sugu na Prof Jay alichoongeza yeye ni katika verse ya tatu.
“Verse ya mwiso ndio imeleta utata watu kuona Chemical anashindana na watu. Siwezi kusema imeleta chuki ila watu wameona kama Chemical kapaniki kuona marapa wa kike wanafanya fresh, hawajui hii ni sanaa sio ya kujisifia na ukiangalia sio ngoma moja mimi kufanya hivi, that its hip hop watu wasiichukulie too person,” amesema Chemical.
Wimbo wa Queen of Dar es Salaam Chemical amechukua verse moja moja pamoja na chorus kutoka kwenye wimbo wa  Prof Jay ‘Bongo Dar es Salaam’, na ile ya Sugu na Balozi ‘Dar DSM.

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.