Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo. Kushoto akizungumza katika mkutano huo.
Hapa wakitiliana saini mkataba huo.
Mkutano ukiendelea.
Hapa mkataba ukiangaliwa baada ya kusainiwa.
Meneja Masoko wa Benki ya Finca, Nicholous John kushoto), akikabidhi jezi kwa Rais wa Klabu hiyo Azimkhan Akber Azimkhan kulia). Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo na Makamu wa Rais wa Dar City Club, Hamidu Zuberi.
Makabidhiano yakiendelea.
Na Dotto Mwaibale
Benki ya FINCA Microfinance leo imesaini mkataba wa udhamini wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 na klabu ya soka ya Dar City F.C.
Mkataba huo uliosainiwa jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya Benki ya FINCA , makubaliano hayo yanajumuisha kuipatia jezi za michezo klabu hiyo pamoja na kuipatia timu fedha za usafiri na mahitaji mengine ya msingi katika msimu ujao wa ligi Daraja la Pili.
Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano Meneja amasoko wa FIINCA, Nicholous John alisema kwamba udhamini huo ni kuthibitisha tena sera ya benki hiyo ya kujikita katika kusaidia wajasiriamali vijana, kuhakikisha wanakua na waje kuwa watu waliofanikiwa katika sekta ya kifedha na hali kadhalika katika jamii kwa ujumla.
“FINCA tunaamini katika kukuza umuhimu wa kukuza uchumi ndani ya jamii, hususani vijana, na ndio maana tulikuwa tayari kukubaliana na juhudi za ziada za vijana hawa baada ya kubaini kwamba wanavyo vipaji vya kuwawezesha kufika mbali kulingana na hali ya michezo ilivyo,” alisema John na kuongeza kwamba wameamua kujumuisha utamaduni wa ujasiriamali katika michezo.
Dar City FC ambayo ilifanikiwa kuingia katika mashindano ya Kombe la Mabingwa wa Shirikisho hivi karibuni inatarakiwa kusafiri hadi Kahama, mkoani Shinyanga ambako itaungana na timu nyingine saba katika ligi ya mabingwa wa mikoa nchini.
Aidha Rais wa Klabu hiyo Azimkhan Akber Azimkhan aliishukuru FINCA kwa ukarimu huo wa msaada akisema kuwa umekuja wakati sahihi na katika kipindi ambacho klabu hiyo inakabiliwa na changamoto za kifedha.
“Tunatoa shukrani nyingi kwa Benki ya FINCA kwa msaada huu uliokuja kwa wakati mwafaka, sasa hivi tuna uhakika kwamba tutafanya vizuri katika mashindano kwa kuwa udhamini huu utatuwezesha kwa kiwango kikubwa kwa timu kuwa na morali na hamasa ya kufanya kazi kwa bidii, “ alisema Azimkhan.
Alifafanua kuwa matayarisho kwa ajili ya mashindano hayo yanajumuisha mahitaji kadhaa na hiyo ni changamoto kwa makampuni mengine, watu binafsi na mashirika katika kuzisaidia timu zinazoibua kwa kutambua umuhimu wake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo wakati akiishukuru FINCA kwa udhamini wake alitoa wito kwa taasisi nyingine za kifedha kuiga mfano maridhawa wa FINCA kwa kuzisaidia klabu nyingine za soka zinazoibukia ndani ya jiji.
No comments:
Post a Comment