Mchekeshaji Steve Nyerere mwenye vipaji vya kuigiza sauti mbalimbali za viongozi, amewataka Watanzania kuacha kumuhusisha kwenye sakata la kutengeneza audio ambayo anasikika malkia wa filamu, Wema Sepetu akizungumza mambo ya faragha na Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Freeman Mbowe.
Mwenyekiti huo wiki hii, aliikataa audio hiyo kwa kusema siyo yake huku akiwataka Wanzania kutulia wakati timu yake ikifanya uchunguzi juu ya sakata hilo.
Akiongea na Jumatano hii, Steve Nyerere amedai kila mtu anajua hawezi kufanya kitendo kama hicho kwaajili ya kumchafua mtu.
“Sio mimi yule na siwezi kufanya kitu kama kile,” alisema Steve. “Ile sauti ukiisikiliza kwa makini utajua sio mimi na siwezi kufanya hivyo,”
Alisema hataki kulizungumzia zaidi sakata hilo kwa kuwa anaweza akaanzisha mjadala mpya kitu ambacho hapendi kitokee.
Muigizaji huyo alihusishwa kwenye tukio hilo baada ya kusikika mtu anayedaiwa kuwa ni Wema akitaja jina lake.
No comments:
Post a Comment