.

HABARI ZA KIJAMII

DC LYANIVA - AFANYA USAFI NA WAKAZI WA BUZA

Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amesheriki katika zoezi la kufanya usafi kila la kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, ambapo amefanya usafi wa pamoja na wanachi wa kata ya Buza mtaa wa Mashine ya maji.
DC Lyaniva ameweza kuzungumza na wananchi wa kata ya buza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM kata ya Buza.
katika mazungumzo yake DC Lyaniva amewasisitiza wananchi kupenda kufanya usafi katika maeneo yao na sio kusubirri serikali ije kuwafanyia usafi, ambapo pia amewahimiza wananchi wa Buza kushirikiana vyema na jeshi la polisi katika suala zima la ulinzi na usalama wa mitaa yote ya kata ya buza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Nassib Mbaga aliwahimiza vijana kupenda kufanya kazi na sio kukaa vijiweni pia aliahidi kudhamini mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi vya vijana ili waweze kujiajili wenyewe.Inline image 1

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.