HABARI ZA KIJAMII

FUTARI YA DIWANI KATA YA MAKURUMLA, KUBENEA ATOA WITO HUU KWA WAKAZI WA UBUNGO

Diwani wa Kata ya Makurumla iliyoko Manispaa ya Wilaya ya Ubungo Omary Kambo, amewasihi waislamu kuendeleza yale mema waliyoyaanza wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani ili kudumisha misingi ya dini na maarisho ya Mtume Muhamad (S.A.W) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Diwani Kambo, ameyanena hayo wakati akifuturisha baadhi ya Waislamu waliojitokeza katika kata hiyo ofisini kwake , wananchi pamoja na baadhi ya Viongozi wa siasa akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya chama cha Chadema, Said Kubenea.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Diwani Kombo, amewashukuru sana Mashekhe pamoja na wananchi wake kwa kujitokeza kwa wingi katika futari hiyo iliyoambatana na dua za kuwaombea walitangulia mbela ya haki na kuliombea Taifa la Tanzania lizidi kudumisha amani iliyopo katika kuleta maendeleo ya Taifa hapa nchini.
Diwani Kombo, amesema kuwa mwezi huu umefundisha mambo mengi ikiwemo jinsi ya kusaidiana kwa wale wenye njaa, pamoja na kukumbushana makatazo yote yaliyoamarishwa katika Dini na kudumisha misingi ya dini ya kislamu katika kuleta usawa wa haki.
"Maisha ya kufunga siku 30 sio kitu rahisi sana, mfungo huu wale waliokuwa wanafunga walipaswa kuwagawia chakula wale wasio na uwezo, kipindi hiki ni kipindi cha kusamaehewa madhambi na kuanza kurasa mpya hapa Munngu huwashukia wanadamu zake kwa masmaha hivyo tunaelekea kuumaliza mfungo huu tuendelee na mema ambayo tulikuwa tukifanya ili tuweze kutafuta pepo na kuishi maisha mazuri akhera"amesema Diwani Kombo
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea, aliwataka mashekhe kipindi cha swala wajitahidi kuombea Taifa la Tanzania pamoja na viongozi wake ikiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloongozwa na Spika wa Bunge Job Ndugai kuliongoza kwa misingi ya haki na demokrasia ili Taifa lipige hatua
Pia Kubenea, amesma kama Bunge halitazingatia mslahi ya umma na kuleta ushabiki wa kisia litawagawa watanzania na kupeleka machafuko ya kisiasa kama yalivyotokea nchi jirani ikiwemo Sudani Kusini na Sudani Kaskazini.
Hata hivyo Kubenea, amesema kuwa, Bunge la sasa linaendeshwa na ushabiki wa kisiasa hivyo ili Taifa lifanikiwe ni lazima wabunge wa Jamhuri ya Muungano kujadili na kungalia mambo ya msingi
"Bunge linatakiwa kujadili mambo ya msingi sio utashi wa kisisa, hivyo ili ili tufanikiwe tunatakiwa turudi katika misingi ya Bunge tujadili mambo ya msingi, ukiangalia asilimia 40 ya fedha zinatoka nje ya nchi lazima tufike wakati tuangalie maslahi mapana ya Taifa,"amesema Kubenea
Mbali na Bunge, Kubenea maeelezea matukio ya kigaidi yanayoendelee kushika kasi Kibiti, akiwaomba Serikali kutatua kwa kukaa na wananchi wenye badala yke waache kutumia nguvu ili kuweza kushinda vita hii dhidi ya manyanyaso wanayofanyiwa ndugu zetu wa K Ibiti, na kama Jeshi litakuwa halijafanikiwa amewashauri kutumia wachunguzi wa Kimataifa ili kufanikisha zoezi hilo.
Kubenea amewasihi viongozi wenzake wasitoe lugha chafu ambazo zinalenga kulimega Taifa wanatakiwa watumie lugha nzuri ili kudumisha misingi ya amani iliyopo hapa nchini.

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.