Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Direct Pay Online Group,Eran Feinsten (kushoto) akionesha namna wanavyotumia mfumo wa mawasiliano kutuma na kupokea fedha katika banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yalioyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi kuanzia tarehe 2 mpaka tarehe 4 Juni. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii(TTB)Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba.
DIRECT PAY ONLINE
GROUP [DPO] MDHAMINI WA KILIFAIR 2017 DARAJA LA PLATINAMU
Direct Pay Online Group ni mdhamini daraja la Platinamu
katika KiliFair 2017
DPO ni moja ya kampuni inayoongoza katika malipo Afrika ikiwa
na operesheni nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Tanzania, Zanzibar, Zambia,
Namibia, Botswana na Afrika Kusini.
HABARI KAMILI-----
|
Shirika
linaloongoza katika kutoa huduma za malipo Direct Pay Online ni mdhamini wa
maonyesho makubwa ya utalii na biashara kanda ya Afrika Mashariki ya KILIFAIR
2017. Maonyesho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Ushirika tarehe 2 hadi 4
mwezi Juni mwaka huu yalikusanya wafanyabiashara zaidi ya 300 kutoka Tanzania
na nchi jirani na kuwa na wageni zaidi ya 3000 kutoka nje na ndani ya nchi.
“Tunajivunia kuwa wadhamini wa kiwango hiki
cha platinamu katika maonyesho makubwa kama haya. Hii ni fursa muhimu kwa
kampuni yetu ya DPO kujitangaza kwa kazi kubwa tunayofanya ya kurahisisha
malipo haswa kwa sekta ya safari,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa DPO Eran
Feinstein.
Katika bidhaa zilizokuwa katika maonyesho
kwende banda la DPO ni pamoja na huduma ya bure inayoitwa MarketPlace ambayo
iko wazi kwa wafanyabiashara na wateja wote wa hoteli, safari, mawakala na
maduka wa DPO wanaotumia tovuti hiyo na huduma nyingine kuuza bidhaa zao na pia
kuwapatia fursa ya kujitangaza ulimwenguni bure. DPO pia ilionyesha jinsi ya
kutumia programu ya DumaPay ambayo inawezesha wafanyabiashara kuwatoza wateja
wao kutumia teknolojia inayosoma kadi kwa usalama mahali popote na muda wowote.
Mteja huweza kulipa kupitia kadi au simu kwa sarafu wanayopendelea.
Fahamu zaidi Kuhusu Direct Pay Online
DPO
kwa sasa inahudumia zaidi ya wateja 20,000 barani Afrika ikiwemo mashirika ya
ndege 50, maelfu ya mahoteli, mawakala wa usafiri na wafanyabiashara wengine wa
mitandaoni na inaendelea kujitanua katika maeneo mapya. DPO inachukua kadi zote
kubwa za malipo ikiwemo,
malipo ya pesa kwa simu na pochi za mitandaoni (e-wallet) na ni kiongozi katika
teknolojia, utoaji huduma kwa urahisi na usalama. Ni mtoa huduma hizi pekee
katika Afrika Mashariki yenye hati ya viwango vya juu ijulikanayo kama PCI DSS
Level 1, ikiwa ni shahada ya juu kabisa katika masuala ya usalama katika malipo
ya kadi ikihakikisha viwango vya juu kabisa vya usalama na usiri wa data za
watumiaji.
Mawasiliano:
DPO Group
Kate Gathii
No comments:
Post a Comment