Tuesday, June 20, 2017

Dk. Kigwangalla “Nasimama na Rais wangu”, afunguka mapambano ya rasilimali za Taifa

Dk. Kigwangalla “Nasimama na Rais wangu”, afunguka mapambano ya rasilimali za Taifa Kupitia ukurasa wa kijamii wa twitter wa Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ameweka wazi kuwa daima ataendelea kupambana dhidi ya rasilimali za umma, kwani amekuwa mwanaharakati kwa muda mrefu. “Tuliopinga wizi wa madini yetu tulibezwa, tulikamatwa kama wezi; tuliswekwa ndani, tulionekana wasaliti. Leo kiko wapi? #NasimamaNaRaisWangu" aliandika Dk. Kigwangalla huku watu mbalimbali wakitoa maoni yao. 

Kwa mujibu wa Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, suala la kupambana na rasilimali za Taifa alilianza miaka mingi kwani miongoni mwa matukio makubwa ni la 2013, ambapo alijitolea kupambana kudai haki tukio lililopelekea kutiwa nguvuni na Jeshi la Polisi. Mtandao huu ulipowasiliana na Dk. Kigwangalla ambaye yupo Bungeni Mjini Dodoma, alibainisha kuwa, katika kupigania maslai Taifa ataendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk. 

Magufuli mwanzo mwisho kwani ni moja ya matunda ya nchi yoyote ile Duniani, kiongozi Mkuu lazima alinde na kupigania rasilimali za nchi, hivyo akiwa Mtanzania na kiongozi mwenye dhamana anaunga juhudi hizo bila kuchola. "Tulipambana na tunaendelea kupambana. 2013/4 Nilipambana na kudai haki kwa wachimbaji wadogowadogo na wale waliokuwa wakitunyonya katika migodi yetu, ikiwemo mgidi wa Resolute uliojulikana kama Nzega Golden Pride Project. 

Tulipambana tulibezwa na hata kulala mahabusu kwa kupambana na rasilimali zetu, leo hii tumepata kiongozi mkuu mwenye uchungu na taifa ili, lazima tumuunge mkono" alieleza Dk. Kigwangalla kwa njia ya simu na mtandao huu. Tazama VIDEO la tukio lingine la Dk. Kigwangalla alivyosimamia masuala ya risilimali Bungeni:
Ujumbe wake huo..
Baadhi ya maoni ya watu
Dk. Kigwangalla akiwa ametiwa nguvuni wakati wa kusimamia haki ulinzi wa migodi jimboni kwake, Nzega, Mkoani Tabora.
Dk. Kigwangalla

No comments: