Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Kikishirikiana na Taasisi
ya za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi kwa Watu Wenye Ulemavu wamelaani
vikali kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi cha kuwapiga na kuwadhalilisha
walemavu wakati wakiwa kwenye madai yao ya msingi. Hayo yamesemwa leo kwenye
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya kituo hicho yaliyopo
kijitonyama jijini dar es salaam.
Akiongea na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
hiyo Bw. David Nyendo alisema kuwa wanasikitishwa na Polisi kwa kuweza kutumia
nguvu kubwa ya kana kwamba wanapambana na majambazi kumbe ni watu wenye
ulemavu. Kujichukulia Sharia mkononi pia ni kosa kwani chombo pekee chenye mamlaka
ya kutoa hukumu ni Mahakama. “Kitendo cha kuwapiga, kuwaburuza na
kuwadharirisha Walemavu ni kinyume cha Sharia na kinafaa kupingwa na kila Mwananchi”.alisema
Hivyo kufuatia yote hayo Jeshi la Polisi limetakiwa kutekeleza
mambo kadhaa ikiwa ni fidia kwa watu wenye ulemavu kwa kuwadhalilisha na kuwaumiza.
Jeshi la Polisi kuacha kutumia nguvu kubwa iliyopitiliza ili
kuweza kulinda haki za walemavu na Raia wa kawaida kwani kufanya hivyo ni
kuvunja misingi ya utoaji haki.
Ndani ya siku saba Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es salaam na
Mkuu wa Jeshi la Polisi kuomba msamaha kwa njia yeyote ile itakayoona ni vema, ikiwa
ni kujitkeza hadharani kuwaomba msamaha
watu wenye Ulemavu na Taifa kwa ujumla kwa kitendo cha udhalilishaji
kilichofanywa na maafisa wake mnamo tarehe 16/6/mwaka huu. Kwani kinyume na
hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya jeshi hilo.
Sanjari na hayo yote Jeshi la Polisi limetakiwa kutoa fidia
ama nafuu kwa waathirika wa shambulizi hilo.
1.
Kutoa Baiskeli za Walemavu 30 ambazo
ziliharibiwa kutokana na shambulio hilo.
2.
Kulipa fidia kwa wale wote waliolipotiwa kupotelewa
na mali zao kama fedha na simu kwenye shambulio hilo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiendelea kchukua Habari kwenye mkutano wa LHRC na HREDP wakitetea haki za walemavu leo jijini Dar es salaam |
No comments:
Post a Comment